Ndege
ya Delta Airlines aina ya Boeing 767-300 ilikua ikipaa urefu wa futi
38,000 angani na kisha ghafla rubani akawasiliana na abiria ili
kuwajulisha kwamba ndege itatua kwa dharura Albuquerque ikitoka Atlanta
kuelekea Los Angeles Marekani.
Mmoja kati ya abiria wa ndege hiyo Jennifer Squires amesema
“nilidhani kuna mtu ameumwa lakini baada ya muda kidogo rubani alisema
sababu ni msukumo wa upepo kusababishia kioo cha mbele ya ndege
kuvunjika kwa nje bila kuvunjika kwa ndani’
“Niliposhuka kwenye ndege niliomba kuona sehemu iliyovunjika na
kupiga picha hii, nashukuru rubani kwa kutushusha salama na kuweza kutoa
habari hii kwa wananchi wengine pia ndege nyingine iliagiziwa kuja
kutufata kutoka Los Angeles” – Jennifer
Post a Comment