
Kama Diamond Platnumz angekutana na Eiden usiku wa kuamkia
Jumamosi ya leo, huenda angemfanya mwanamke huyo wa kizungu kuwa mwenye
furaha kuliko watu wote duniani. Mwanamke huyo ambaye usiku huo alikuwa
akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 32, anadai
alisafiri kutoka nchini Rwanda kuja jijini Dar es Salaam ili amtafute
hitmaker huyo wa ‘Number One’ amuimbie wimbo maalum wa siku ya kuzaliwa.
Bahati mbaya, mara tu baada ya kutumbuiza kwenye show ya Road to
MAMA, aliwahi ndege ya kwenda jijini London, Uingereza kuwahi show yake
na Ommy Dimpoz na kuizima ndoto ya Eiden.
“Mimi ni shabiki mkubwa zaidi wa Diamond duniani,” Eiden aliiambia
Bongo5. “I want him to sing me happy birthday cause I am his number one
fan and I’m not married I have no kids and I am not ashamed. I just love
him and I think I feel like he needs to meet me, If he doesn’t meet me
his life is not gonna be the same. I am incredible, if he doesn’t know
me he is just gonna be a poor person in the world.”
Kazi kwako Chibu.
Post a Comment