Ni
kawaida kuona makocha wa jinsia ya kiume wakiwa wanafundisha timu za
mpira wa miguu za wanawake, lakini ni mara chache sana tumewahi
kushuhudia kocha wa kike akiwa anaifundisha timu ya wanaume.
Lakini klabu ya ligi daraja la kwanza
ya Ufaransa Clermont imeweka historia mpya kwenye soka la nchi hiyo kwa
kumtangaza mwanamama Helena Costa kuwa kocha wao mpya kuanzia msimu
ujao, na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza kufundisha soka la hadhi ya
juu nchini Ufaransa.
Costa, 36, alikuwa kocha wa timu ya taifa ya
wanawake ya Irani tangu mwaka 2012 lakini sasa amekubali kumrithi Regis
Brouard kwenye klabu ya Clermont.
Helena ambaye ni raia wa Ureno, aliwahi
kufanya kazi kama kocha mkuu wa kituo cha soka cha klabu ya Benfica na
timu kadhaa nyingine nchini Ureno, ambapo aliweza kushinda makombe
kadhaa. Pia aliwahi kuifundisha timu ya wanawake ya taifa ya Qatar.
Post a Comment