Jay Z na Beyonce baada ya “Ugomvi” na SOLANGE. #WhatJayZSaidToSolange

20140513-101833.jpg
Jay Z na Beyonce wakiwa wamekaa “courtside” pamoja wakiangalia “Play Off” ya ‘Brooklyn Nets’ na Miami ndani ya NYC usiku uliopita … Hii inaonyesha kuwa wapo kwenye “Same Boat” kutokana na ugomvi uliotokea tarehe 4 May 2014 kwenye Lift kati ya ‘Jay Z’ na mdogo wake ‘Beyonce’ ajulikanae kama ‘Solange Knowles’, ugomvi huo ambao ulitokea kwenye lift wakiwa wanaelekea kwenye ‘after party’ baada ya kutoka kwenye event ya ‘MET Gala’ siku hiyo na kuweza kutoka kwenye public siku ya jana na kwenda “Viral” kwenye mitandao ya kijamii mpaka sasa naona #Trending inayoendelea kwenye twitter bado ‘Solange’ na ‘Jay Z’ wanaongoza kama #WhatJayZSaidToSolange sababu inaonekana kabisa jamii haijui sababu ya mwanadada huyo kutaka kupigana na shemeji wake mbele ya dadake wakiwa kwenye Lift.
Wakiwa wamekaa kwenye ‘Front Row’ kama kawaida wapenzi hao huku rafiki wa karibu wa Hov mchezaji LeBron James akiwa anapata talk na couple hao ambao waliingia kwenye game wakati wa ’2nd Quarter’ wakiwa na nyuso za furaha na kuonekana kila kitu kipo sawa. Kwa muhibu wa walioshuhudia baada ya kutoka kwenye Lift hiyo familia hiyo ilijigawa kwa Beyonce kuondoka pamoja na mdogo wake ‘Solange’ na Jay aliondoka kivyake.
Wana familia hao hakuna hata mmoja alieongelea kuhusu swala hilo na kwa muonekano walioonekana katika game hiyo usiku uliopita inajieleza zaidi kuwa hakuna tatizo linaloendelea na kuacha #WhatJayZSaidToSolange na yote yaliyosemwa au kusababisha ugomvi huo naona yamebaki ndani ya Carter & Knowles Family.
Thats What Black People Do, Stays in a Family.

Post a Comment

Previous Post Next Post