Belle 9 ni miongoni mwa wasanii wakali nchini ambao hawajawahi
kuwa na bahati na tuzo za Kilimanjaro na mwaka huu bahati haikuwa kwake
pia. Kukosa kwake tuzo kumewaumiza mashabiki wake akiwemo Elizabeth
Michael aka Lulu.
Kupitia Twitter, Lulu ameandika: Namshukuru Mungu kwa ushindi wa
@FidQ sasa mwaka mtakaompa Tuzo Belle 9 nitatoa sadaka
kabisaaaaa.#KTMA.”
Lulu akimkabidhi tuzo Vanessa Mdee kwenye usiku wa KTMA weekend iliyopita
Kauli ya Lulu imempa moyo Belle 9 ambaye ameiambia Bongo5:
“Nachoweza kusema hapo Lulu kuna kitu amekiona kwenye muziki wangu
ndio maana akasema kauli hiyo. Hii inanipa nguvu zaidi ya kuongeza
juhudi zaidi kwa kile ninachokifanya ili nifike mbali zaidi. Kama Lulu
kasema hivyo hebu jiulize ni wangapi? Wanatambani kitu kama
hicho,kwahiyo ni dhahiri kuna watu wengi sana wanafuatilia muziki
wangu.”
Post a Comment