KINDA LA MAN UNITED, JAMES WILSON LAFANYA MAMBO MAKUBWA GIGGS AKISHINDA 3-1 OLD TRAFFORD

MANCHESTER United wamemaliza mechi za Old Traffod kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Hull City usiku huu.
Kocha mkuu wa muda wa Man United, Ryan Giggs katika mchezo wa leo aliamua kuwapa nafasi wachezaji vijana wa klabu hiyo Tom Lawrence na James Wilson.Pia Michael Keane alikaa benchi tayari kwa kuwaonesha kazi Hull.
Wilson mwenye miaka 18 mapema aliwaaminisha mashabiki wa Man United kuwa anaujua mpira baada ya kuifungia bao katika dakika ya 31, na baadaye dakika ya 61 aliandika bao la pili kimiani kabla ya mkongwe Robin Van Persia kufunga bao la tatu katika dakika ya 86.
Bao la Hull limefungwa katika dakika ya Fryatt dakika ya 63.
Mwanzo mzuri: James Wilson aliifungia Man United mabao mawili katika mechi yake ya kwanza usiku huu
Wilson (kulia) akishangilia bao lake na Nemanja Vidic
Kijana huyo wa ajabu ni nani?
Umri: 18
Alipozaliwa: Staffordshire
Mechi za kwanza: Wilson anapenda mechi za kwanza. Mshambuliaji huyo alifunga bao katika mechi yake ya kwanza kwenye akademi ya Man United ya miaka 15.Pia alifunga bao lake la kwanza kwenye mechi yake ya kwanza katika kikosi cha timu ya taifa ya England chini ya miaka 19 mwaka 2013.
Ukweli wa kufurahisha: Wilson alisaini mkataba wa kitaaluma na Man United siku yake ya kuzaliwa ya mwaka wa 17 mwaka 2012.
Ryan Giggs alishinda mataji mawili ya ligi, moja la FA na kombe moja la ligi kabla ya Wilsom kuzaliwa.
James Wilson 
Akiwa na miaka 15, Wilson alifunga bao lake la kwanza katika mchezo wa kwanza dhidi ya Everton na ikiwa imepita miaka mitatu sasa amefanya kitu kama hicho tena, lakini safari hii amefunga katika mechi yake ya kwanza kwenye mchezo wa ligi kuu.
Giggs amempatia nafasi kijana huyo mwenye miaka 18 kucheza mechi yake ya kwanza na ameweza kuwaaminisha Man United kuwa anajua soka baada ya kufunga bao kipindi cha kwanza.
Mashabiki wa United walimfahamu mshambuliaji huyu kijana siku alipowekwa benchi na Moyes kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Newcastle mwezi aprili mwaka huu, wakati huo wote Rooney na Van Persie hawakuwepo.
Wilson hakuingia uwanjani, lakini aliwashangaza wengi kwa kupangwa kwake katika mechi kubwa kama hiyo.
Cha kufurahisha, Wilson aliamua kuvaa soksi na viatu vyeuusi katika mechi yake ya kwanza Old Trafford usiku huu, kitu ambacho si cha kawaida kwa soka la sasa ambapo wachezaji wengi wanapenda kuvaa viatu na soksi za rangi.
Mtoto wa shule: Tofauti na vijana wa soka la kisasa siku hizi, Wilson aliingia uwanjani akiwa na viatu vyeusi.
Ndoto: Mkongwe wa United Rio Ferdinand amemsifu Wilson kwa kiwango alichoonesha katika mechi yake ya kwanza


Shambulizi: Wilson alifunga bao lake baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Adnan Januzaj
Wilson (kushoto) akiifungia Man United bao la kuongoza

Post a Comment

Previous Post Next Post