SAA chache baada ya kocha wa Yanga,
Mholanzi, Hans van Der Pluijm kuweka wazi kwamba hataendelea kuinoa timu
hiyo msimu ujao, tayari Kocha Luc Eymael raia wa Ubelgiji ametangaza
kuwa yupo tayari kuchukua mikoba ya Mholanzi huyo.
Pluijm amemaliza mkataba wake wa miezi sita na jana alitangaza kutimkia
Saudi Arabia alikopata ofa nzuri zaidi kuinoa Al Shoala SC inayoshiriki
ligi kuu ya huko kwa msimu mmoja.

Eymael ambaye awali alikuwa akiwania nafasi ya kuinoa Yanga pamoja na Pluijm, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, tayari ameshavunja mkataba na klabu yake ya Rayon SC ya Rwanda, hivyo ameikaribisha Yanga kwa ajili ya mazungumzo.
Eymael aliyevunja mkataba wa mwaka mmoja uliobaki na klabu yake hiyo, amesema anatamani kuifundisha Yanga na yupo tayari kupokea ofa yao kwa ajili ya kuiletea mafanikio zaidi msimu ujao.
“Nimevunja mkataba na Rayon, kuna vitu vingi vimenifanya nichukue uamuzi huo ila timu iliyo mbele yangu kwa sasa ninayotazamia kuifundisha ni Yanga.
“Natamani kukinoa kikosi cha Yanga na kama watakuwa tayari basi nipo tayari kwa ajili ya mazungumzo na kuchukua nafasi ya Pluijm,” alisema Eymael.
Rayon iliyokuwa mikononi mwa Eymael, imefanikiwa kumaliza ligi msimu uliopita ikiwa kwenye nafasi ya pili huku ikizidiwa pointi mbili na mabingwa wa Ligi Kuu ya Rwanda,
Post a Comment