‘Kubadili magari kunanipa furaha’ anunua Mark X mpya - Nay wa Mitego

Msanii wa Hip Hop, Nay Wa Mitego amenunua gari lake jipya aina ya Mark X kwa gharama ya shilingi milioni 20 huku akidai kuwa anajisikia furaha anapobadili magari ya kutembelea.
Gari mpya Mark X ya Nay Wa Mitego
Gari mpya Mark X ya Nay Wa Mitego

Akizungumza na Bongo5, Nay amesema amekuwa akinunuA magari ya aina mbalimbali mara kwa mara kwakuwa ndio hobby yake.
“Kumiliki magari tofauti tofauti ni hulka ya mtu, unajua kuna watu wanapenda kucheza mpira,wengine nini,lakini mimi napenda magari,hii Mark X nimenunua pesa ndogo kama milioni 20 na ni gari yangu ya saba tangu nianze kumiliki magari yangu mwenyewe ila ambayo nayamiliki kwa sasa ni mawili,” amesema.
Pia Nay amedai kuna siku ataamua kuwaonesha Watanzania mali zake zote

Post a Comment

Previous Post Next Post