MAADHIMISHO YA SIKU YA ALBINO DUNIANI YAFANYIKA JIJINI DAR .



Umati wa watu waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Albino Duniani wakiwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akitoa hotuba fupi.
Balozi wa Uturuki nchini, Ali Dovutoglu akitoa salamu zake.
Albino wakiwa kwenye foleni tayari kwa kupima afya zao bure. Wanachama wa Chama cha Albino Tanzania wakinadi bidhaa zao.
Mmoja wa wanaharakati wanaopinga unyanyaswaji wa albino akigawa riboni zenye ujumbe wa kutetea  unasemao: “Watu wenye ualbino ni binadamu kama sisi.”
Riboni zenye ujumbe.
Na Waandishi Wetu
Maadhimisho ya Siku ya Albino Duniani yamefanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakitaifa na kimataifa.

Mgeni rasmi wa maadhimisho hayo yaliyokuwa yanafikia kilele leo alikuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete yalihudhuriwa pia na Balozi wa Uturuki nchini Hon. Ali Dovutoglu.

Pamoja na shamrashamra nyingine maadhimisho hayo yaliambatana na huduma za afya kama upimaji wa kansa ya ngozi na macho kwa albino zilizotolewa bure kuendana na kauli mbiu ya maadhimisho hayo isemayo: HAKI YA AFYA, HAKI YA UHAI.

(Picha: Chande Abdallah na Shani Ramadhani /GPL)

Post a Comment

Previous Post Next Post