Marekani imesema inapeleka vifaa
vya uchunguzi nchini Nigeria kusaidia katika juhudi za kuwatafuta
wasichana wanaozuiliwa na kundi la Boko Haram.
Wasichana hao walitekwa nyara kutoka shule moja Kusini mwa eneo la Borno mwezi mmoja uliopita.Msemaji wa Rais Obama Jay Carney amesema kikosi cha maafisa 30 kiko nchini Nigeria tayari kushiriki juhudi hizo.
Amesema msaada huo wa Marekani kutoka wizara za mambo ya nje na ulinzi na pia kutoka idara ya uchunguzi ya FBI.
Hatua hiyo imechukuliwa wakati baadhi ya Jamaa za wasichana waliotekwa nyara wakielezea majonzi baada ya kutazama kanda ya video iliyotolewa na kundi hilo.
Mzazi Nigeria
"Ni heri watuonyeshe maiti za wasichana wetu badala ya kuwazuilia vichakani. Hili ni swala la hisia za ubinadam. Sisi hatuwezi kwenda kuwaokoa, wanajeshi hawawezi kwenda huko. Ni heri kutumia nguvu. Tukiona maiti zao mioyo yetu itakua huru"
Kwenye kanda hiyo ya video kiongozi wa Boko Haram , Abubakar Shekau anasikika akiambia serikali ya Nigeria yuko tayari kubadilishana baadhi ya wasichana hao na wafuasi wake waliofungwa jela.
Hatahivyo wizara ya mambo ya ndani ya Nigeria imetupilia mbali pendekezo hilo.
Seneta Ali Ndume kutoka eneo ambapo wasichana hao walitekwa nyara anaisihi serikali kulegeza msimamo.
Post a Comment