
Mbunge
wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere (Chadema) ameeleza kufurahishwa na Serikali
kwa kufanyia kazi maombi yote ambaye amekuwa akiyawasilisha bungeni, miongoni
mwake ikiwa ni pamoja na wananchi wa Kwimba kupatiwa huduma za kijamii.
Leticia
ambaye alikuwa akichangia makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka
wa fedha 2014/15, alisema juzi kwamba aliomba maji, walimu, umeme na mawaziri
husika wamempatia .
“Naipongeza
Serikali ya CCM kwa kutekeleza yale yote ambayo nimekuwa nikiyapigania
bungeni.,” alisema Leticia ambaye alisisitiza umuhimu wa wananchi kuchangia
miradi ya maendeleo.
Akizungumzia
maombi yake kuhusu walimu, alisema halmashauri ya wilaya ya Kwimba imepatiwa
walimu 300.
Hata
hivyo aliendelea kuwasilisha maombi ya vitabu kwa ajili ya shule wilayani humo.
Alisema idadi hiyo ya walimu ni sawa na kuvaa suruali bila kufunga
vifungo.
Leticia
ambaye uchangiaji ulionekana kuduwaza upande wa upinzani wakati upande wa CCM
wakishangilia, alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo pamoja
na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Seleman Mzee kwa uchapakazi wao.
Baada
ya kuchangia, alishangiliwa na wabunge wa CCM na Spika Anne Makinda alisema,
“Kushukuru ni kuomba…na hiyo ndiyo siasa.”
Katika
hatua nyingine Mbunge wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya
(CUF) alikosoa hatua ya serikali kuonesha silaha zake katika maadhimisho
ya miaka 50 ya Muungano. Alishutumu kitendo hicho akisema si haki nchi
kuonesha silaha zake hadharani.
Hata
hivyo Mbunge wa Manyoni Mashariki, John Chiligati (CCM), alimpa taarifa akisema
kilichooneshwa ni kitu kidogo. Chiligati alimwambia kuonesha silaha ni
jambo la kawaida duniani
Post a Comment