
Mbwana ambaye anakichezea kikosi cha TP Mazembe cha DR Congo, alisema kiungo wa Zimbabwe, Kudakwashe Mahachi, ndiye alikuwa tatizo kwao.
Kwa wale waliotazama mchezo huo, Mahachi alikuwa amevaa jezi namba 11 na riboni mkononi ambapo alikuwa akiisumbua sana safu ya ulinzi mara kadhaa.
Akizungumza na , Samatta alisema Stars ilijitahidi kutokana na hadhi ya Zimbabwe kuwa kubwa kwani wameshiriki michuano ya Afcon mwaka jana, hata hivyo uelewano baina yao uliwasaidia sana kupata ushindi huo, japo ni kiduchu.
“Kuna jamaa sikumkariri vizuri na jezi yake, lakini alikuwa akitumia sana mguu wa kushoto, mwenye rangi nyeupe kichwani, kweli alitusumbua mara kadhaa, ingawa tunashukuru tumepata ushindi.
“Ilikuwa mechi ngumu, lakini nafikiri kwa kuwa tunaongea lugha moja (Kiswahili), ilichangia kuelewana zaidi na kucheza kwa umakini kutokana na wapinzani wetu kuonekana kubadilika baadaye na kutushambulia,” alisema nyota huyo.
Post a Comment