Mirror wa Endless Fame kufanya yake ndani ya The Playlist ya Times FM Jumapili hii

Mwimbaji wa Bongo Flava anaefanya kazi chini ya kampuni ya Endless Fame ya Wema Sepetu, Mirror aka Kioo atakuwa katika kipindi cha The Playlist cha 100.5 Times FM Jumapili hii (June 1).
MIRROR THE PLAYLIST
Mkali huyo wa ‘Baby’ ambaye hivi sasa ameachia pini jipya alilolibatiza jina la ‘Kolokolo’ atazicheza ngoma tano kali anazozipenda zaidi na kuzielezea, pia atajibu maswali ya kichokozi yaliyonyooshwa na rula ya Omary Tambwe aka Lil Ommy, mtangazaji wa kipindi hicho.
Pamoja na mengi atakayohusika nayo, Mirror atazungumzia uhusiano wake na marehemu Ngwair, kazi alizofanya nae na mipango waliyopanga na member huyo wa Chemba Squad. The Playlist ambayo siku zote inawapa nafasi wasikilizaji kuzifahamu ngoma tano kali wanazozipenda mastaa wanaowakubali, kinakuwa hewani kupitia 100.5 Times Fm kila Jumapili kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa kumi na moja kamili jioni.
Unaweza kuwasiliana au kufuatilia show ya The Playlist wiki hii kupitia mitandao ya kijamii @timesfmtz @lilommy @mirror26
@petitman_wakuache

Post a Comment

Previous Post Next Post