
Mratibu
wa mashindano ya Miss Uni-College Temeke, Silas Michael (katikati)
akiwatambulisha baadhi ya warembo ambao Jumamosi watapanda jukwaani
kwenye ukumbi wa Dar Live kuwania nafasi ya mshindi wa kwanza.
Mashindano hayo yatapambwa na burudani kutoka kwa msanii wa muziki wa
kizazi kipya hapa nchini, Snura Mushi “Mamaa Majanga” .
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Snura Mushi “Mamaa Majanga”
atapamba mashindano ya Miss Uni-College Temeke 2014 yaliyopangwa
kufanyika kwenye ukumbi wa Dar Live Mbagala Jumamosi.
Mbali
ya Snura ambaye atafanya shoo kwa kutumbuiza nyimbo zake zote kwa mara
ya kwanza, pia bingwa wa masindano ya Tikisa dance 2012 Hassan Jigoro
naye atapamba mashindano hayo yatakayoshirikisha juma ya warembo 12
kutoka vyuo mbali mbali vya elimu ya juu vilivyomo manispaa ya Temeke.
Warembo
hao ni Martha Mashaka, Sarah Joseph, Diana Joachim Kato, Theola
Benedict, Eliana Lucumay, Nyangeta Kuboja, Naila Haroun Yusuph, Martha
Manzawa, Susan Joseph, Karen Swai, Sarah Jacob na Flora Kimaro.
Warembo
hao wanatoka vyuo vya Kumbukumbu ya ya Mwalimu Mwalimu Nyerere, Chuo
Cha Utalii, TIA na Magogoni. Mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh 300,000 na
vocha ya manunuzi yenye thamani ya Sh250,000 kwenye dula la Robby One
fashion,wakati mshindi wa pili atapata Sh250,000 na vocha ya manunuzi ya
Sh250,000 na wa tatu Sh 200,000 na wanne na wa tano watapata sh100,000
kila mmoja.
Pia
kutakuwa na zwadi ya kifuta jasho ya Sh50,000 kwa warembo waliobaki na
zawadi ya simu tatu za Huwawei kwa warembo watakaoonyesha nidhamu ya
hali ya juu, kujiamini na mrembo bora katika muonekano pichani.
Mashindano
hayo yamedhaminiwa na Continental outdoor, Global Publishers, Robby One
fashion, Clouds Media group, Leluu Saloon, New Habari Corporation,Mesho
decoration, Millard Ayo, salut5, Huwawei , Lamada Hotel, Shamoo Hotel.
Post a Comment