Missy Temeke
Mkurugenzi wa KWETU Fashions hatimaye amefunguka kutokana na maoni ya
watu waliopinga tangazo lake la kwamba amealikwa kwenye maonyesho ya
tamaduni yanayofanywa na Balozi mbalimbali Washington, DC na kubeba jina
la PASSPORT DC yakiwa chini ya Caltural Tourism DC na yanayoadhimishwa
kila mwaka wakati huu wa majira ya spring.
Missy Temeke aliongea na Vijimambo May 5, 2014, na kusema "wanaosema
sijaalikwa sio kweli muasisi wa PASSPORT DC alinifuata baada ya kuona
meza yangu siku ya maadhimisho ya sherehe ya miaka 50 ya Muungano na
kuniomba barua pepe yangu na kwamba angependa niwe mmoja ya washiriki
kwa kuiwakilisha Tanzania na pia kama naweza kuonyesha mitindo ya
mbalimbali ya nguo za KWETU Fashions." Baada ya Hapo mawasiliano
yalianza na mimi kuweka tangazo langu kwenye Vijimambo na waosha vinywa
kuanza kusukutua bila mswaki huku wengi wakidai nadanganya na wengine
kulazimisha kuleta vitu vyao bila kujua meza zimetolewa kwa hesabu.
Mimi Barua
yangu ya mwaliko hii hapa mchana kweupe na naomba aliyejileta kwa kudai
maonesho yalikuwa ya wazi naomba nae alete barua yake ya mwaliko hapa
Post a Comment