V
Stiviano ambae ni mrembo alievujisha mazungumzo ya simu ya mkononi kati
yake na bilionea Mmarekani mmiliki wa timu maarufu ya mpira wa kikapu
ya L.A Clippers Donald Sterling alietoa maneno ya kibaguzi kwa watu
weusi, ameongea kwa mara ya kwanza.
Kwenye dakika 14 za interview ya ABC amesema Donald ambae kwa sasa
anajisikia mpweke, anatakiwa kuomba msamaha japo haijulikani ni lini ila
Mungu pekee ndio anajua.
Anasema uhusiano wa kimapenzi ulianza wakati akifanya kazi chini ya
bilionea huyu na ni mapenzi ambayo ilifikia kipindi watu walikua
wanamshangaa au wanashindwa kuelewa uhusiano wao.
V Stiviano amesema bado anampenda Sterling ila hayuko nae inlove,
anampenda kama baba…. Sterling kiumri ana miaka 80 na yeye ana umri wa
miaka 31.
V anasema amekua msaidizi wa Donald na kwamba chanzo cha yeye
kutembea akiwa amejiziba uso toka hii ishu itokee ni ili asiongee na
Waandishi ambao wamekua wakimuandama wasimpate, hakutaka kuongea
chochote sababu alikua na machungu na kwamba ni ngumu kuona mtu
unaemjali akiwa kwenye maumivu.
Anasema Waandishi wa habari wamekua wakikosea na kuuliza watu kuhusu
yeye lakini kosa kubwa wanalolifanya ni kwamba wanauliza watu ambao sio
sahihi kuulizwa kuhusu yeye. (wrong people)
Pamoja na yote yaliyotokea V ameushangaza ulimwengu kwa kumtetea
Sterling kwamba sio mbaguzi na kama angekua mbaguzi basi asingetoa
msaada ambao ameutoa mpaka sasa kwa watu mbalimbali… ‘kupitia matendo
yake ameonyesha kwamba sio mbaguzi na ni mtu mkarimu’
Kwenye
sentensi nyingine V anasema sehemu ya sauti iliyosikika Donald akitoa
maneno ya kibaguzi kuhusu watu weusi ni dakika 15 tu kati ya saa kadhaa
za maongezi ambayo dunia haijazisikia.
<iframe width="560" height="315" src="//www.youtube.com/embed/MWCxXHyLZp4" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>
Kutokana na maneno ya kibaguzi, Donald amefungiwa maisha
kutojihusisha na timu yake wala kufanya chochote kwenye timu hiyo ambayo
pia ina wachezaji wengi weusi.
Imeripotiwa kwamba V Stiviano kama nyumba ndogo ya Donald, alipewa
jumba la kifahari pamoja na magari ya kifahari yasiyopungua matatu
likiwemo Ferarri.
Post a Comment