Waombolezaji
Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard akichangia |
Msafara wa kuekea kuzika |
Msafara kuelekea kuzika |
Msafara kuelekea makaburini |
Baadhi ya wadau wakielekea kuzika |
Diwani wa kata ya Mvinjeni Frank Nyalusi Chadema akiweka udongo |
Ndugu wakiweka mashada |
Ndugu wa kalolo kutoka Kenya akiweka shada |
Mstahiki meya Amani Mwamwindi akiweka shada la maua |
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza akiweka shada |
Mbunge wa
jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiweka shada la maua
katika kaburi la kada maarufu wa Chadema mkoa wa Iringa Gervas Kalolo
wakati wa mazishi yaliyofanyika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa
Na Francis Godwin Blog
*******
MAZISHI ya
kada maarufu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Gervas
Kalolo yatikisa mji wa Iringa baada baada ya magari zaidi ya 100 na
boda boda na bajaji zaidi ya 200 kupamba msafara wa mazishi hayo jana
Mazishi
hayo ambayo yaliongozwa na mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji
Peter Msigwa yalionyesha kuvunja rekodi ya mazishi yaliyopata
kufanyika katika mji wa Iringa .
Awali
utaratibu wa mazishi hayo ulitaka kuvurugika kutokana na vijana wa
Chadema kuanza kuzomea makaburini wakati Mc wa mazishi hayo wakati
akitambulisha taratibu za watoa salam mbali mbali na kumtaka
mwakilishi wa chama cha mapinduzi (CCM) huku akishindwa kumtaja
mwakilishi wa Chadema na kuishia kusema kutakuwa na mwakilishi wa
chama bila kutaja jina la chama husika .
Hata hivyo
baada ya MC huyo kufuatwa na diwani wa Chadema kata ya Mvinjeni Frank
Nyalusi na kumlazimisha kutaja jina la Chadema badala ya kuishia
kutaja chama bila jina lake ,ndipo alipolazimika kuepusha vurugu kwa
kutaja jina la chama cha Chadema na kupelekea kuibuka kwa shangwe
katika msiba huo.
Mbali ya
kuibua shangwe kwa kuimba wimbo wa Chadema Chadema alisimama mbunge
wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Msigwa ambae pia alishangiliwa kwa
nyimbo hizo za Chadema .
Akizungumza
katika mazishi hayo mbunge Msigwa mbali ya kumshukuru mstahiki meya
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Aman Mwamwindi na viongozi wa CCM
kwa kushirikiana na chama katika mazishi hayo bado alisema kuwa
kimsingi siasa katika msiba huwekwa kando.
Mbunge
Msigwa alisema kuwa kiongozi yeyote na mtu yeyote mchango wake
hupimwa kwa matendo yake na kuwa umati wa wananchi waliojitokeza katika
mazishi hayo ni wazi kuwa Kalolo alikuwa ni kiongozi wa mfano katika
jamii na kuwa Chadema itamuenzi kwa kusimamia msimamo wake wa kupinga
ufisadi .
Kwa upande
wake mwakilishi wa CCM katika mazishi hayo Shadrack Mkusa alisema
kuwa Kalolo ambae alipata kuwa diwani wa kata ya Miyombini Kitanzini
kabla ya kushindwa katika kura za maoni na kujiunga na Chadema.
Alisema kuwa
Kalolo anakumbukwa kwa mengi ambao amepata kuyafanya likiwemo la
kusimamia hoja zake katika vikao vya madiwani pamoja na kujitolea
kusaidia watoto yatima katika kata yake.
CHANZO: ALLYSHAMS BLOG
Post a Comment