
Ikiwa kama maadhinisho
ya kila mwaka baada ya watanzania wengi sana kupoteza maisha yao katika
janga hilo na kuacha majonzi makubwa katika familia zao. Mwanamitindo
“Flavianna Matata” ambae na yeye ni kati ya watanzania ambao walikumbwa
zaidi na msiba huo wa watanzania wote ambapo mwanadada huyo alimpoteza
MAMA yake mzazi akiwa safarini ndani ya “MV Bukoba” ajali iliyotokea
zaidi ya Miaka 18 iliyopita. Makumbusho haya yalihudhuliwa na wasanii
wakiwemo AY, viongozi wa serikali, wafiwa, walionusurika na wananchi
wengine wa maeneo hayo mjini Mwanza.
Mwanadada Flaviana Matata ambae amekuwa mstari wa mbele sana
kuhusiana na kumbukumbu hizi kila mwaka huacha shughuli zake zote na
kufika mjini Mwanza kuweza kuhani msiba wa mama yake na wengine wote
waliofariki kwenye janga hilo. Akisindikizwa na Baba yake Mzazi “Mzee
Matata”, Mwanadada huyu sio kuhani tu msiba, ila ni mmoja kati ya watu
ambao wapo makini sana kuhakikisha janga kama hili halitokei tena sababu
amekuwa mstari wa mbele kabisa kutoa misaada mbali mbali kuweza
kuimalisha usalama wa abiria wasafirio kutumia vivuko vya mjini, ambapo
Flaviana ameshawahi kutoa “Life Jackets” kwa ajili ya vivuko
vinavyotumika kwenye njia hiyo.


Baba Mzazi wa Flaviana Matata.






Flaviana akiwa na mmoja kati ya walionusurika kwenye ajali hiyo.







PICHA Kwa Hisani ya Slide VISUALS
Post a Comment