Mwenyekiti
wa Young Africans Bw Yusuf Manji amesema kuondoka kwa wachezaji wao
wawili Didier Kavumbagu na Frank Domayo sio mwisho wa timu ya Yanga,
kwani uongozi wake unaendelea na mipango ya kuhakikisha inasajli
wachezaji wengine wazuri ambao wataisadia timu kwenye msimu ujao kwa
kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi.
Akiongea
na waandishi wa habari makao makuu ya klabu leo, Manji amesema
yameongelewa mengi sana kwa kipindi cha mwezi mmoja ambao hakuwepo
nchini kwa ajili ya kazi zake binafsi lakini sasa amerejea na maandalizi
ya msimu ujao yameshaanza.
Kuondoka
kwa Kavumbagu ni kutokana na kuchelewa kwa majibu ya TFF juu ya idadi
ya wachezaji wageni kwa msimu mpya, huku Domayo ambae tangu mwaka jana
aliombwa kuongeza mkataba alikua akisema anamsubiria mjomba wake ndipo
aweze kufanya hivyo.
Post a Comment