PROFESA WA HIP HOP ALIYEKUMBUKWA KWA TUZO ZA KILI - FID Q

NDANI ya gemu la Hip Hop Bongo, ni vichwa vichache sana ambavyo vimebaki tangu miaka ya 90 hadi sasa, miongoni mwao ni mkali kutoka Jiji la Mwanza ambaye alizaliwa Agosti 13, 1982, Farid Kubanda ’Ngosha The Swagga Don’ au Fid Q.
Fid Q ’Ngosha The Swagga Don’ wakati akihojiwa na Global TV Online.
Ni fundi aliyeitendea haki midundo ya ngoma kali kama Mwanza Mwanza, Proffesional, Agosti 13 na nyingine kibao.
Juzikati pande za Mlimani City, ulimwengu wa muziki Bongo ulishuhudia akipewa tuzo mbili kwa mpigo; Msanii Bora wa Hip Hop na Mtunzi Bora wa Hip Hop, hii ni ishara tosha kwamba jamaa muziki wake unaendelea kuthaminiwa.
Licha ya kuanza gemu kitambo, hadi sasa jamaa ana albamu mbili tu mkononi, Vina Mwanzo Kati na Mwisho na Propaganda na kwa sasa yupo mbioni kutoka na albamu ya tatu itakayoenda kwa jina la KitaaOLOJIA.Nilimtafuta Fid Q na kuzungumza naye mengi yahusuyo maisha yake kimuziki, jiunge nami:
Ulishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji Salama Jabir?
Hilo swala siyo kweli, hizo tetesi sishangai kusikia kwako hata kwa Watanzania wengi wameshawahi kuhoji na zaidi mama yake, pia alishawahi kuhisi hivyo nadhani ni urafiki wetu wa karibu ambao ulikuwa mkubwa zaidi na ilikuwa ni ngumu kuamini kama tunaweza kuwa marafiki wa kawaida, ieleweke kuwa Salama ni mshikaji wangu tu na hakuna mambo mengine yoyote ya faragha.

Kwa nini watu huwa wanalalamika unapokosa tuzo za Hip Hop?
Mimi sifanyi muziki wa Hip Hop mimi ni Hip Hop mwenyewe umeshanielewa vizuri.

Fid Q akiwa kwenye pozi na baadhi ya wafanyakazi wa GPL.
Ninaposema hivyo ni kwamba nime ‘inspire’ asilimia 98 ya wanaofanya Hip Hop kwa hiyo inapotokea mtu aliyewapa hamasa akashindwa kupata hata tuzo huwa inawauma na ndiyo maana ushindi wangu ulikuwa ni wa kila Mtanzania.
Mtanzania wa sasa hivi amebadilika sana tofauti na yule wa zamani ambaye unamwambia kitu hakifanyii utafiti, wa siku hizi unamwambia kitu anakifanyia utafiti mpaka anakijua.
Unawazungumziaje wanaosema umependelewa tuzo kwa mwaka huu?
Januari 26, mwaka 2008  niliachia wimbo ulioitwa Ni Hayo tu nikiwa nimeshirikiana na Langa (marehemu) pamoja na Profesa Jay na nikajipatia Tuzo ya Killi kwa wimbo huo ikiwa Wimbo Bora wa Kushirikiana.

Sikuwa mbali sana na tuzo kwani nilishirikiana na watu wengi ambao waliingia katika tuzo na kuchukuwa, nakumbuka nilishawahi kukutana na Witness ambapo nilimpa mdundo wangu mwenyewe ukiwa pamoja na kiitikio cha wimbo wa Ziro ambao ulichukuwa tuzo ya Channel O.
Achana na huo, nikashirikiana na JCB katika wimbo wa Ukisikia Paa ukachukuwa tuzo ikiwa ni Wimbo Bora Wa Hip Hop. Nilikuwa sipewi tuzo lakini kazi nilizokuwa nikishirikiana zilikuwa zikipata.
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikishindanishwa na sura nyingine nyingi katika vinyang’anyiro lakini nilikuwa ndani ya Circle ileile japokuwa nilikuwa sipati tuzo.
Ukiwa unawakilisha Mwanza umejipanga vipi kuwainua wasanii wa mkoa wako?
Swali zuri, namiliki darasa lenye watu 50 linaloitwa Ujamaa Darasa na next wiki nazindua video mpya ya Ujamaa Hip Hop Darasa na kama mambo yakienda vizuri natarajia kufungua tawi Mwanza.

Nawakilisha Mwanza siyo kwa sababu nipo Dar, hapana!  Yaani nawakilisha Mwanza na dunia nzima kwa sababu najivunia kuwa ‘Mwanzania’ yaani kama Mwanza ingekuwa nchi kama ilivyo Tanzania ningeitwa ‘Mwanzanian’.
...Fid na Pamela Daffa wa Global TV Online.
Nini maana ya Utamaduni na Hip Hop Darasa?
Hip Hop Darasa ni darasa langu ambalo nawafundisha wanafunzi fikra mbadala katika utendaji na maamuzi yao.

Utamaduni ni kitu chochote ambacho kinawasilisha asili ya jamii husika kwa hiyo kama mimi ni mweusi asili yangu ni Mwafrika. Sasa hivi nafanya albamu ya KitaaOLOJIA ambayo inamaana ya elimu ambayo mimi naipata mtaani na ‘kushare’ na nyinyi.
Vitu vingi ambavyo nakuwa naimba siyo nimefundishwa shuleni. Sijaribu kusema kuwa shuleni wako wrong, hapana najaribu kusema kuwa mtu unaweza kuwa nje ya shule na ukawafundisha watu wa mtaani wakaelewa vilevile.
Vipi matarajio yako ya kuoa?
Kiukweli kabisa naomba niwe muwazi, natarajia kuoa hivi karibuni lakini nakumbana na vikwazo vingi sana coz nina mtoto.

Unajua unapokuwa na mwanamke halafu una mtoto wa nje inakuwa ni ngumu kumfundisha mtoto aweze kuelewa kuwa siyo mama yake. Kwa hiyo hicho ndicho kitu nakutana nacho lakini inshaallah Mwenyezi Mungu nimemtanguliza mbele nimempata ambaye ananifaa na muelewa.
Una bifu na Weusi?
No, siwezi kuwa nao. Nipo nao muda mrefu na haiwezi kutokea hivyo. Wasanii wengi wanapenda kujiingiza bifu katika ‘media’ ili wafahamike zaidi kwangu mimi hakuna kitu chochote na tena naomba niwaambie mimi sina bifu na mtu yeyote na kama ingekuwa bifu ningekuwa na Rado ambaye mpaka aliniandikia wimbo wa Usiulize.

Nilichomwambia Rado ni kuwa kibao ni kizuri hata ‘presenters’ niliwaambia ni wimbo mzuri waendelee kuupiga.
- GPL

Post a Comment

Previous Post Next Post