Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage.JAMBO limezua jambo! Imefahamika wazi kuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, amegoma kutoa shilingi milioni 100 za klabu hiyo kwa ajili ya usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara mapema Agosti, mwaka huu.
Simba ipo kwenye kampeni za uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Juni 29
na habari zilizopo ni kuwa, kiasi hicho cha fedha kimepatikana kutokana
na malipo ya kodi ya majengo ya kibiashara yaliyopangishwa kwenye jengo
la klabu hiyo yaliyopo Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Awali, mtoa taarifa aliliambia gazeti hili kuwa, Rage anazo fedha
hizo lakini amegoma kuzitoa kwa vigogo wawili wa Simba ambapo wengine ni
wagombea katika uchaguzi wa sasa wakidai kuwa wanahitaji kwa ajili ya
kufanya usajili.
“Walipokutana na mwenyekiti waliomba kiasi cha shilingi milioni 100
kwa ajili ya usajili na kufanya maboresho ya baadhi ya nafasi zenye
upungufu kwa mujibu wa ripoti ya kocha wetu (Zdravko Logarusic).
“Fedha hizo wanazozitaka zimetokana na malipo ya kodi ya kila mwaka
tunayoyapata Simba kwa wapangaji wetu tuliowapangisha kwenye jengo letu
tunalolimiliki lililopo Msimbazi.
“Mwenyekiti ameshikilia msimamo wa kutotoa fedha hizo na kusisitiza
kuwa, atazikabidhi kwa viongozi wapya watakaoingia madarakani na siyo
wanaomaliza madaraka yao ya uongozi,” alisema mtoa taarifa.
Alipotafutwa Rage kuzungumzia hilo, alikiri kuwepo kwa watu hao bila ya kuwataja majina na kusema walitaka awape fedha kwa ajili ya usajili wa msimu ujao.
Alipotafutwa Rage kuzungumzia hilo, alikiri kuwepo kwa watu hao bila ya kuwataja majina na kusema walitaka awape fedha kwa ajili ya usajili wa msimu ujao.
“Kweli kabisa nimekataa kutoa fedha hizo za usajili walizokuwa wanazitaka hao watu.
“Wao wasiwe na haraka na fedha hizo, wasubiri watazikuta tu na isitoshe dirisha la usajili bado halijafunguliwa, mambo kama hayo yanahitaji umakini wa hali ya juu, hasa katika kipindi hiki ambacho namaliza madaraka yangu.

“Isitoshe hao watu wenyewe siyo viongozi wa Simba, wenyewe wanataka
kutumia fedha hizi kujipigia kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu, kitua
ambacho nimekikataa,” alisema Rage.
Post a Comment