Mkurugenzi
wa Uendeshaji toka wakala wa huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) bw.
Naftal Singwejo akieleza kwa waandishi wa habari kuhusu mfumo mpya wa
kielektroniki utakaotumika katika kutoa huduma ya mafuta kwa magari ya
Serikali na mitambo ili kuongeza tija katika utoaji wa huduma hiyo kwa
Taasisi ,Wakala na Wizara zote .kushoto ni Mkurugenzi Himili Biashara
Bw. Malik Aram. (FS)
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali yaanza kutekeleza mradi wa kufunga mfumo wa kielektroniki kujaza mafuta magari na mitambo ya taasisi za Umma ili kuongeza tija katika utoaji huduma hiyo kote nchini.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa wakala wa Huduma ya Ununuzi
Serikalini (GPSA) bw. Naftal Singwejo wakati wa mkutano na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua
Singwejo amesema mradi huo utashirikisha Wizara,Taasisi zote za
Umma,Wakala na Idara zinazojitegemea ambazo kwa mujibu wa sheria ya
ununuzi wa Umma na 7 ya Mwaka 2011 sura ya 410 kifungu cha 56 zinatumia
huduma hiyo toka kwa wakala huo.
“Hatua za
awali za utekelezaji wa mradi huu zitahusisha kufungwa kifaa maalum
(identification tag) katika mlango wa tanki la gari au mtambo “alisema
Singwejo
Akizungumzia faida za mfumo huo, Singwejo alisema hakutakuwa na mfanyakazi (Pump Attendant) wa kuweka mafuta katika gari au mtambo na hivyo huduma hiyo itapatikana kwa haraka na hivyo kuongeza tija.
Akizungumzia faida za mfumo huo, Singwejo alisema hakutakuwa na mfanyakazi (Pump Attendant) wa kuweka mafuta katika gari au mtambo na hivyo huduma hiyo itapatikana kwa haraka na hivyo kuongeza tija.
Faida
nyingine ni kuwa taarifa ya matumizi ya mafuta ya chombo cha umma
itapatikana kwa wakati kwa njia ya mtandao na hivyo maamuzi sahihi
kufanyika juu ya matumizi ya mafuta kwa chombo husika.
Aidha, Singwejo alibainisha kuwa mfumo huo utaondoa kabisa udanganyifu wa matumizi ya mafuta katika magari na mitambo kwa taasisi za umma na kutoa nafasi kwa chombo kilichodhibitika tu kuweza kupata huduma ya mafuta.
Aidha, Singwejo alibainisha kuwa mfumo huo utaondoa kabisa udanganyifu wa matumizi ya mafuta katika magari na mitambo kwa taasisi za umma na kutoa nafasi kwa chombo kilichodhibitika tu kuweza kupata huduma ya mafuta.
Naye
Mkurugenzi Himili Biashara Bw. Malik Aram alisema kuwa mfumo huo ni wa
kisasa ambao unatumika katika nchi zilizoendelea na majaribio ya mfumo
huo hapa Tanzania yatafanyika katika kituo cha Kurasini mwishoni mwa
mwezi Julai, 2014 ambapo hadi sasa mfumo huo umeanza kusimikwa katika
kituo hicho.
Bw. Malik
aliongeza kuwa baada ya kukamilika kwa mfumo huu katika kituo cha
Mafuta cha kurasini katika mwaka huu wa fedha katika mwaka ujao wa fedha
mfumo huo utafungwa katika Mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Mbeya, na
Mwanza.
Serikali
ilianzisha wakala wa Huduma ya ununuzi Serikalini (GPSA) ili kudhibiti
matumizi ya fedha za umma yanayofanyika kupitia ununuzi wa vifaa
mbalimbali na mafuta kwa ajili ya magari na mitambo ya umma, hivyo
mfumo huu ni moja ya hatua za utekelezaji wa mpango huo kamambe wa kuwa
na matumizi ya rasilimali za umma wenye tija.
Post a Comment