
Akiwa ni miongoni mwa wasanii wenye majina yao Tanzania na hata
kwenye nchi jirani, mwimbaji Shaa atarudi tena kwenye spika zako na
kwenye TV yako hivi karibuni akiwa na sound mpya ya single yake ambayo
mazingira ya kiswahili/Kitanzania yamehusika ndani yake.
Hii ni May 18 2014 wakati akiifanya video maeneo ya Manzese Dar es
salaam kupitia mikono ya Director anaepewa heshima kila siku kutokana na
mikono yake kuhusika kuzipeleka mbali video za kitanzania…. Adam Juma
kutoka Next level.
Wakati ukiwa tayari kupokea video mpya unaweza kutumia sekunde zako
kucheki jinsi utengenezwaji wenyewe ulivyofanyika kisha uache maoni yako
yatakayosomwa baadae jioni.
Post a Comment