Uongozi
wa Klabu ya Young Africans umeshangazwa na taarifa zilizoandikwa kwenye
mojawapo ya vyombo vya habari juu ya Wanachama wa Tawi la Tandale
kusema hawatambui kufutwa kwa Tawi lao ni za Ubabaishaji.
Mnamo Mei 04, 2014 Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans Bw Yusuf
Manji alitangaza kulifuta Tawi la Tandale kutokana na kua chanzo cha
migogoro ndani ya klabu kwa kipindi cha mrefu, ili hali likiwa halina
hadhi ya kuwa Tawi Kamili.
Kufutwa kwa Tawi la Tandale kunatokana na kutotimiza idadi ya
wanachama mia moja (100) kama inavyojieleza kwenye Katiba ya Yanga SC,
Ibara ya 6, kipengele cha 4 "Kutakuwa na uundaji wa matawi katika maeneo
mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi. Kiwango cha chini ya idadi ya
wanachama ambao wanaweza kunda tawi kisipungue watu mia moja (100)".
Ibara ya 13, kipengele cha 2 kinasema " Kutolipa ada zake za
uanachama kwa muda wa miezi sita mfululizo bila ya sababu maalum
inayokubalika na Kamati ya Utendaji"
Baadhi ya Wanachama walijifuta uanchama wao kutokana na kushindwa
kulipia ada zao za uanachana kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita, kama
inavyojieleza kwenye Katiba kwamba mwanachama asipolipia ada yake zaidi
ya miezi sita moja kwa moja anajifuta uanachama wake.
Hivyo Uongozi wa klabu ya Yanga SC unaomba Umma na Wanachama wake Duniani kote watambue kuwa Tawi la Tandale lilifutwa kwa kutokana na kutokidhi vigezo, huku wanachama wake wengine watano wakijifuta uanachama kwa kushindwa kulipia ada zao kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.
Mwisho wanachama wa klabu ya Yanga SC wanaombwa kulipia ada zao za uanchama mapema kabla ya muda wao kumalizika ili waweze kushiriki mkutano mkuu wa marekebisho ya Katiba utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi - Oysterbay Juni Mosi 2014.
Beno Njovu
Katibu Mkuu - Yanga SC
Mei 23, 2014

Post a Comment