TAMBWE BYEBYE SIMBA SC

Mshambuliaji Hamis Tambwe akishangilia.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba, Mrundi Amissi Tambwe, anawaniwa na timu kutoka nchi za Oman, Msumbiji kwa ajili ya kwenda kuzitumikia katika ligi za nchi hizo ingawa haijatajwa, timu gani inahitaji saini ya straika huyo.
Mashabiki wa Simba SC wakiwa katika mashamsham.
Awali baada ya ligi kumalizika, timu kadhaa hapa nyumbani zilionyesha nia ya kutaka kumsajili kinara huyo wa mabao wa Ligi Kuu Bara, ikiwemo Azam.
Chanzo cha karibu cha mchezaji huyo kilisema kuwa timu nyingi zinatamani kumsajili kinara huyo wa mabao ambaye kwa sasa anaitumikia klabu yake ya Simba, zikiwemo za nchini Oman, Msumbiji.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa, timu ambazo zinamhitaji mchezaji huyo zimetangaza dau nono endapo tu atakuwa tayari.

“Tambwe amebahatika kupata ofa katika timu za huko Oman na Msumbiji na wamemuahidi kumlipa zaidi ya anavyolipwa Simba,” kilisema.
Championi Jumamosi lilimtafuta mchezaji huyo ambaye kwa sasa yuko nchini Botswana akiitumikia timu yake ya taifa na alisema kuwa yeye bado ni mchezaji halali wa Simba na ana mkataba, hivyo hawezi kuzungumzia suala hilo.
“Mimi ni mchezaji halali wa Simba na nina mkataba wangu pale, hayo mambo ya timu zingine kunihitaji siwezi kuzungumzia suala hilo,” alisema Tambwe.

- GPL

Post a Comment

Previous Post Next Post