Filamu ya “The Amazing Spider-Man 2″ imekamata nafasi ya kwanza
kwenye box office (majumba ya sinema) nchini Marekani katika weekend ya
May 2-4, 2014.
Ikiwa na mastaa Andrew Garfield, Emma Stone na Jamie Foxx, filamu
hiyo iliingiza dola milioni 35.5 ijumaa peke yake na kufikisha jumla ya
dola milioni 91 siku tatu tangu itoke.
Baada ya kukaa kwenye nafasi ya kwanza wiki iliyopita, filamu ya
Cameron Diaz na Nicki Minaj, “The Other Woman” imeshuka hadi nafasi ya
pili. Filamu hiyo ya comedy imeingiza dola milioni 4.8 siku ya Ijumaa na
kumaliza weekend hii ikiwa imeingiza jumla ya dola milioni 15.1.
Filamu zingine zilizopo kwenye tano bora ni “Heaven is for Real”
($8.5 million), “Captain America:The Winter Soldier” ($7.6 million) na
“Rio 2″ ($7.5 million)
Post a Comment