Tuzo za kimataifa za CNN kwa waandishi wa habari Afrika 2014 zazinduliwa.

 Tuzo za kimataifa zinazotolewa na CNN kwa ushirikiano na Multichoice ‘CNN MultiChoice African Journalist 2014 Awards zimezinduliwa rasmi ambapo waandishi wa habari wa Afrika watapata nafasi ya kuziwania.
Tuzo hizo zinalenga katika kuwatunuku waandishi wa habari za Afrika ambao wamefanya vizuri zaidi katika kukusanya na kuripoti habari zao kwa mwaka huu.

 Mwaka huu njia ya kuiunga na shindano hilo kwa waandishi wa habari imerahisishwa zaidi ambapo mwandishi anatakiwa kujaza form ambazo zinapatikana kwenye tovuti maalum yawww.cnnmcaja.cnn.com 
 “Tangu mwanzo kabisa, tuzo hizi zimevumbua na kuwatunuku waandishi wa habari bora zaidi katika bara hili. Kwa habari nyingi zaidi za Afrika sasa hivi wanaweza kushare nasi kazi zao, tunatarajia hata ingizo jipya la kazi bora zaidi zilizotukuka.” Amesema Tonny Maddox, Mkurugenzi Mtendaji wa CNN International.

 Hii ni fursa pia kwa waandishi wa habari wa Tanzania.  
 Hivi ni baadhi ya vipengele vitavyoshindaniwa/ vitakavyoangaliwa mwaka huu: 
 Culture Award
 The Coca-Cola Company Economics & Business Award
 GE Energy & Infrastructure Award (*NEW*)
 Environment Award
 MSD Health & Medical Award
 News Impact Award (*NEW*)
 Mohamed Amin Photographic Award
 Press Freedom Award
 Sport Reporting Award
 Francophone General News Awards – Electronic media &

Post a Comment

Previous Post Next Post