Tukiwa bado kwenye mtafaruku wa ‘Racism’ uliotokea nchini marekani kusababisha mpaka Rais wa nchi hiyo Mr President Barack Obama kuzungumza kuwa ni tabia mbovu kwa Zee hilo la kizungu Donald Sterling ambalo ni Owner wa NBA Basketball Team “L.A Clippers” kuzungumza na kimada wake kwenye simu ni kiasi gani hapendi watu weusi na hataki waje kuangalia mechi za timu yake. Donald ambae kwa sasa yupo katika wakati mgumu sana baada ya wasanii wengi weusi wa nchini humo akiwemo Magic Johnson, Lil Wayne, Rihanna, Lebron James, Meek Mill, Kevin Hurt na wengine wengi kupinga kabisa tabia hiyo na kukataza fans kusupport team hiyo la sivyo kwa kuokoa team hiyo lazima “Babu hilo baguzi” liuze team hiyo.
Baada ya vyombo vya habari pamoja na mashabiki wa timu hiyo pamoja mashabiki wa NBA nchini marekani kumtaka Donald Sterling auze timu hiyo sababu si wachezaji wala mashabiki wanamtaka kuwa mmiliki wa timu hiyo baada ya ubaguzi wa rangi aliouonyesha siku chache zilizopita, mastaa wengi wa nchini Marekani wameonyesha nia ya kununua timu hiyo akiwemo mwanamama tajiri duniani OPRAH Winfrey, music mogul Sean ‘Diddy’ Combs, mpigana masumbwi Floyd Mayweather na mcheza filamu nchini humo Matt Damon.
Post a Comment