
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine.
KLABU ya Yanga ipo katika hatua za mwisho kumpandisha kizimbani Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine.
Yanga ipo kwenye hatua za mwisho za mchakato huo kutokana na
kubainika kuna upotevu wa mamilioni ya fedha wakati Mwesigwa akiwa
katibu mkuu wa Yanga.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa, uongozi wa
Yanga chini ya mwenyekiti Yusuf Manji, umelisimamia zoezi hilo chini ya
wakaguzi wa fedha ambao wamegundua upotevu wa mamilioni hayo ya fedha
wakati Mwesigwa akiwa katibu enzi za utawala wa Lloyd Nchunga.
Kwa mujibu wa Katiba ya Yanga, uongozi hauwezi kushtaki, badala yake
unatakiwa kuwasilisha ripoti hiyo kwa baraza la wadhamini chini ya Mama
Fatma Karume ambao ndiyo wamiliki wa klabu.
“Uongozi uliopo madarakani hivi sasa umebaini kuwepo kwa upotevu wa
mamilioni katika kipindi ambacho Mwesigwa alikuwa Yanga. Hiyo ni baada
ya uongozi wa Yanga kupiga mahesabu na kugundulika mamilioni yamepotea,
suala ambalo linajadiliwa sasa ni kumpandisha kizimbani na wadhamini
ndiyo wataamua,” kilieleza chanzo.
Alipotafutwa Mwesigwa jana kuzungumzia hilo, alisema: “Sijui na sina
taarifa zozote kuhusiana na hilo na nisingependa kulizungumzia kwa sasa.
“Pia sipo tayari kuzungumzia kesi yangu niliyowafungulia Yanga, ni vyema ukawauliza wenyewe, nisingependa kuzungumza sana, ninaomba unitafute baadaye kwa ajili ya kuzungumza zaidi kwani muda huu nipo ‘busy’ na majukumu yangu ya kazi.”
“Pia sipo tayari kuzungumzia kesi yangu niliyowafungulia Yanga, ni vyema ukawauliza wenyewe, nisingependa kuzungumza sana, ninaomba unitafute baadaye kwa ajili ya kuzungumza zaidi kwani muda huu nipo ‘busy’ na majukumu yangu ya kazi.”
Post a Comment