![]() |
Justin Bourque mtuhumiwa aliyekamatwa
akihusishwa na yhuma za mauaji ya askari polisi watatu wa Canada Reuters |
Na Emmanuel Richard Makundi
Polisi nchini Canada imetangaza kuwa inamshikilia raia mmoja
anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya polisi watatu na kujeruhi wengine
kadhaa kwenye eneo la Moncton mjini New Brunswick.
Polisi kwenye mji wa New Brunswick kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter
leo asubuhi wameandika kuwa Justin Bourque alikamatwa usiku wa kuamkia
leo kwenye eneo la Moncton.
Taarifa ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu imetolewa baada ya kufanyika kwa
operesheni kubwa na ya kina na polisi wa Canada kuendesha msako wa
kumkamata Bourque.
Shule na ofisi za Serikali zilikuwa zimefungwa kwenye mji huo na
wananchi walitakiwa kutotembea hovyo usiku na kujifungia majumbani mwao
kwakuwa mtuhumiwa huyu alikuwa amejihami kwa silaha nzito.
Kwenye taarifa yao, Polisi kwenye mji wa Moncton wameataka wananchi hivi
sasa kutoka kwenye nyumba zao kwakuwa tishio la usalama limemalizwa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hili wamesema kuwa walishuhudia Polisi wakimkamata mtuhumiwa huyu na kumchukua kwa gari.
Source: kiswahili.rfi.fr/ulaya
Post a Comment