Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Kikosi
cha Taifa Stars kinaingia tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu)
ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya
Afrika dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es
Salaam.
Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku
tatu jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa
programu ya Kocha Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka
huu.
Wachezaji
wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula,
Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram
Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na
Pato Ngonyani.
Wengine
ni Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas
Mkude, Said Juma, Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco,
Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa
na Mwegane
Post a Comment