SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limesema linajipanga kuhakikisha Taifa Stars
inaifunga Msumbiji katika mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika
(Afcon 2015) utakaopigwa wiki mbili zijazo.
Stars imefanikiwa kuitoa Zimbabwe katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 3-2 na sasa inaisubiri Msumbiji na kama ikiing’oa, itatinga kwenye hatua ya makundi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa alisema shirikisho hilo lina jukumu kubwa la kuipatia mahitaji muhimu timu hiyo ili iweze kushinda mchezo huo unaofuata.
“Ni faraja kwa Watanzania wote kufuatia ushindi wa Stars, sasa muhimu kwetu ni kufanikiwa kuitoa Msumbiji.
“Tunahitaji kufanya jitihada za hali ya juu kuhakikisha wachezaji wanapata mahitaji yote muhimu ili waweze kufanya vema katika mechi hiyo ambayo itakuwa na ushindani.
“Kwa sasa sijajua kama kambi itavunjwa au itaendelea kwa kuwa mwenye mamlaka ya kuvunja kambi ni kocha,” alisema Mwesigwa.
Stars ikiitoa Msumbiji, itaingia kwenye Kundi F ambalo tayari lina timu za Cape Verde, Zambia na Niger.

Post a Comment