
Serikali ya Rwanda imedaiwa kuwazuia kupita nchini humo baadhi ya askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliotoka kukisambaratisha kikundi cha waasi wa M23 kilichokuwa Jamhuri ya Kimokrasia ya Kongo (DRC) .....
Kwa
mujibu wa chanzo chetu cha habari kilichozungumza jana na
MTANZANIA Jumatatu kimedai wanajeshi hao walitakiwa kuanza
safari leo kuja nchini kupitia Rwanda lakini walizuiliwa bila
sababu za msingi.
Chanzo hicho kilisema: "Hali
ya usalama kati ya Tanzania na Rwanda sio nzuri hata
kidogo,Wanajeshi waliomaliza majukumu yao nchini Kongo walikuwa
waanze safari yao kurudi Tanzania kesho ( leo ) kwa kupitia
Rwanda, lakini katika hali isiyo ya kawaida Rwanda wamekataa
kupitisha askari hao nchini mwao.
"Mungu
jalia viongozi wetu hekima na busara katika kuamua suala hili
zito kwa kuwa kama tutaingia katika vita wanaoteseka ni
watoto, wanawake na wazee ambao hawana uwezo wa kwenda kuishi
nje ya nchi, sala na dua zinahitajika sana kwa kuwa Mungu ndo
kila kitu," mwisho wa kunukuu
Akizungumzia
suala hilo, msemaji wa JWTZ,Luteni Kanali Erick Komba alisema
hafahamu kama wanajeshi hao walikuwa wameanza kurejea nyumbani,
hivyo apewe muda hadi atakapofika ofisini leo ndipo atahakiki
taarifa hizo.....
Mgogoro
wa Tanzania na Rwanda ulianza kufukuta baada ya Rais Kikwete
kumshauri Rais Kagame wa Rwanda azungumze na waasi wa serikali
hiyo wanaofahamika kama FDLR, ambapo Kagame aligoma na kuanza
kumtolea maneno ya kashifa Rais Kikwete.....
Hata
hivyo, hali ilizidi kuwa mbaya baada ya M23 kusambaratishwa na
JWTZ walioungana na wanajeshi wengine wa vikosi vya Umoja wa
Mataifa (MUNUSCO).
M23
ni kikundi kilichodaiwa kuundwa na askari wa makabila ya
Rwanda, jambo linalopingwa vikali na Rais Kagame.....
Katika
hatua nyingine, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa
mataifa, Benard Membe alikiri kuwapo kwa uhusiano mbaya kati ya
Tanzania na Rwanda.Kauli hiyo aliitoa bungeni mjini Dodoma hivi
karibuni alipowasilisha bajeti ya makadirio ya mapato na
matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha wa 2014/ 2015.
Alisema uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa mbaya kwa sababu kuu mbili kubwa.
"Ni
kweli tuna uhusiano mbaya na Rwanda, kwanza tunaogopana kwa
kuwa kila upande mmoja ukiongea na hasimu wa mwenzake
inaonekana kama kuna hujuma inataka kufanywa.
"Pili
kuna watu wanapeleka maneno ya chokochoko.Pia M23 ni
wanamgambo wa Rwanda na kuna ushahidi kwamba Rwanda ilipeleka
wanajeshi kuwasaidia wakati wa mapigano na serikali ya DRC
yakiendelea, ushahidi huo upo," alisema Membe
Tanzania
ina historia iliyotukuka katika ukombozi wa nchi za kusini
mwa jangwa la Sahara na ndio maana ilichaguliwa kuongoza
majeshi ya kulinda amani DRC
Mwaka
2008, makamanda na wapiganaji wa JWTZ waliongoza vikosi vya
washirika katika kazi ngumu ya kumng'oa kanali Bacar wa Visiwa
vya Comoro na Anjouan.
Uamuzi
wa AU kuipa kazi hiyo Tanzania kuongoza mapambano hayo
haukuwa wa bahati mbaya, bali ulitokana na kutambua kuwa ni
nchi iliyoshiriki na kufanikiwa katika vita mbalimbali ya
ukombozi
CHANZO: GAZETI LA MTANZANIA JUMATATU.
CHANZO: GAZETI LA MTANZANIA JUMATATU.

Post a Comment