
Hayo yalisemwa bungeni mjini hapa
jana na Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile (CCM).
Majaliwa alisema watumishi hao waliokamatwa na kuhusishwa na dawa hizo,
walikamatwa katika kipindi cha mwaka 2012 hadi mwaka 2013.
Alisema watumishi hao walisimamishwa kazi na kisha kushitakiwa
mahakamani, ambapo baada ya kesi zao kusikilizwa, wapo waliofungwa magerezani
na kufukuzwa kazi. Baadhi ya watumishi hao, kesi zao bado zinaendelea
mahakamani.
Majaliwa alieleza kuwa mikakati inayochukuliwa na Serikali ili kukomesha
biashara ya dawa za kulevya ni pamoja na: Kuundwa kwa Kikosi Kazi cha Kupambana na Biashara ya Dawa
za Kulevya mwaka 2006, Kuendelea kutoa elimu kwa umma, hususan vijana kuhusu
athari zitokanazo na dawa za kulevya
na Kutoa huduma ya tiba kwa
watumiaji wa dawa za kulevya aina ya heroin, hasa kwa wanaojidunga.
Mikakati mingine ni Kuongeza uangalizi wa karibu katika maeneo ya
mipaka, yanayotumiwa kuingiza dawa za kulevya, kama vile viwanja vya ndege,
bandari na mipaka ya nchi kavu; Kutunga
sheria mpya ya kupambana na kuzuia biashara ya dawa za kulevya, itakayoanzisha
chombo kipya chenye mamlaka ya kukamata, kuchunguza na kupeleleza masuala
yanayohusiana na udhibiti wa dawa za kulevya nchini.
Majaliwa alisema pamoja na mikakati iliyopo na jitihada zinazofanyika,
changamoto za kupambana na biashara hiyo ni nyingi.
Aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano katika mapambano haya kwa kufichua
wahalifu na kuwapeleka waathirika wa dawa za kulevya katika vituo vya ushauri
nasaha na matibabu, kupata huduma.
Katika swali lake, Ndugulile alitaka kujua watumishi wa vitengo
vinavyodhibiti dawa za kulevya, wamekamatwa au kuhusishwa na dawa za kulevya,
hatua zilizochukuliwa dhidi yao na mikakati ya Serikali kukomesha biashara
hiyo.
Post a Comment