Kujipenyeza kwa al-Shabaab kwenye serikali ya Somalia kwaibua tahadhari mpya ya usalama

Na Fuad Ahmed, Mogadishu
Raia wa Somalia na wachambuzi wamerejeshwa nyuma na maono kwamba mwanaume anayefanya kazi ndani ya eneo la makaazi ya raisi ya Villa Somalia alisaidia al-Shabaab kupita katika vituo kadhaa vya ukaguzi wakati kikundi hicho cha wanamgambo kiliposhambulia eneo hilo wiki lililopita.

Askari wa Somalia akipita kwenye jengo lililoharibika wakati akipiga doria katika mtaa wa Mogadishu tarehe1 5 Julai, 2014. Usalama katika mji mkuu umeimarishwa kufuatia shambulio la al-Shabaab katika eneo la makazi ya rais wa Somalia tarehe 8 Julai. [Mohamed Abdiwahab/AFP]

Serikali ikaonyesha kwamba ilimkamata mwanaume huyo, Hassan Muhiyadin Hassan, baada ya kuwa alijeruhiwa kidogo katika shambulio hilo.

Katika mahojiano na Televisheni ya Taifa la Somalia (SNTV) inayoendeshwa na serikali tarehe 10 Julai, Hassan, ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye kituo cha Hormuud Telecom katika Villa Somalia, alikiri kuwa alikuwa akifanya kazi ya al-Shabaab kwa kipindi karibia cha miaka miwili.

Hassan aliiambia SNTV kwamba alisaidia kukusanya taarifa kwenye maeneo muhimu ya al-Shabaab huko Mogadishu, kama vile hoteli na majengo ya serikali, na alitoa taarifa hizo kwa al-Shabaab kuhusiana na hasara iliyoingiwa na serikali pale ambapo al-Shabaab ilifanya shambulio la kigaidi.

Hassan Muhiyadin Hassan wakati wa mahojiano yaliyofanyika tarehe 10 Julai na Televisheni ya Taifa la Somalia (SNTV) ambapo alikiri kusaidia al-Shabaab. [Radio Mogadishu]

Hassan alisema aliajiriwa na shemeji yake wa kiume, Abdirasaq Said Ibrahim, ambaye alimjua kwamba alikuwa mwanachama wa al-Shabaab.


"Alianza kunipigia simu mwaka mmoja na nusu uliopita akinitaka niwasaidie. Nilimweleza [yeye] kwamba ninafanya kazi kwenye kampuni na kuwa nisingeweza kufanya kazi kama hiyo," Hassan alisema.

"[Abdirasaq] aliniambia kwamba kazi hiyo siyo kama ninavyoifikiria. Aliniambia 'tutakuwa tukiongea kupitia simu, huendi kunifanyia kitu kingine chochote,'" Hassan alisema, akiongezea kwamba alikubali lakini akiomba mawasiliano yake yote yafanywe kupitia shemeji yake wa kiume.

Akigundua njia ya kienyeji ambayo al-Shabaab iliweza kupata taarifa chache alisema, "Lilikuwa jambo la kawaida kuulizwa kuhusu watu binafsi, lakini kulikuwa hakuna ripoti ya kila siku iliyowasilishwa." Waziri wa Ulinzi alikuwa mmoja wa maofisa wa serikali ambaye al-Shabaab ilijaribu kupata taarifa, alisema.

Wakati akikiri kuwa alitoa taarifa kabla ya shambulio la hoteli za Maka al-Mukarama na Oriental, Hassan alikana kujua kuhusu mpango wa al-Shabaab kabla. "Watu hao hawakuambii lengo lao, Wanalisetiri," alisema. "Huwa wanakutaka kwenda kuangalia eneo hilo. Mara unapokwenda hapo, unaripoti unachoona."

Hassan alisema al-Shabaab ililipa nusu ya malipo ya gari lake -- gari alilotumia katika shambulio la Villa Somalia -- na wangemlipa dola 200 kwa awamu.

Mafunzo yaliyopatikana

Maelezo ya Hassan inaonyesha ufanisi na urahisi wa al-Shabaab wa kupata taarifa na kuonyesha kuwa ni hatua mbele ya shirika la upelelezi la serikali ya Somalia, alisema Hassan Sheikh Ali, mchambuzi wa masuala ya usalama mwenye makazi Mogadishu.

"Vita huanza na taarifa. Kama unakuwa na taarifa kuhusu watu uanaopigana nao, utashinda vita hivyo," Ali aliiambia Sabahi.

"Mtu anayepeleleza ni hatari sana kuliko hata mtu mwenye silaha ambaye anafanya shambulio," alisema, akiongezea kwamba serikali imejiweka yenyewe katika uwezekano kwa sababu watu wengi mno wenye ufikivu muhimu hawakuhakikiwa vya kutosha na wanaweza kulengwa na al-Shabaab kwa lengo la kuwaajiri.

Aliyaomba mashirika kupitia mara moja historia ya kila mtu ambaye anatumia mitandao ya serikali.

Idara za usalama pia zinapaswa kuchukua ukurasa kutoka sehemu ya al-Shabaab na kutafuta njia za kupenyeza kwenye mtandao wa kundi la wanamgambo, alisema.

"Kama al-Shabaab, idara za usalama lazima zisambaze na kupokea taarifa kutoka ndani ya al-Shabaab," Ali alisema, akiongeza kwamba serikali inapaswa kutoa kipaumbele kuwekeza fedha zaidi katika kujenga na kudumisha mtandao wa watoa habari wa al-Shabaab.

Taarifa ambazo ziliwakamata wafanyakazi wa al-Shabaab kama vile Hassan ni muhimu, alisema, kwa kuwa zinasaidia idara za usalama kuelewa vizuri jinsi ya kupambana na kundi la wanamgambo. "Wakati idara za usalama zinapokea aina hii ya taarifa inabidi zichukue hatua na kuweka mikakati mapya ya kupambana na [al-Shabaab]," alisema.

Wafanyakazi wa serikali lazima wachunguzwe

Jenerali mstaafu Mohamed Nur Galal, aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi katika utawala wa Mohamed Siad Barre, alisema ufichuaji wa waovu wa ndani unaonyesha kwamba mfumo wa usalama wa serikali uko katika kusambaratika.

"Wafanyakazi wa serikali hawakuwa wanachunguzwa na wamekuwa wakiajiriwa kwa kuzingatia ukoo, na sasa al-Shabaab wamejipenyeza," aliiambia Sabahi. "Kwa hiyo, watu hao, viongozi wa serikali, hawawezi kuulinda mji kabisa."

"Viongozi wa juu hawana hata uelewa wa kutambua al-Shabaab kama wanapita kwao kwa sababu idara ya intelijensia haikujengwa katika namna ambayo inaongoza katika uelewa huo," alisema.

Galal alionyesha wasiwasi wake kwamba idara nyingine za serikali zinaweza kuwa na wafanyakazi ambao wana uhusiano na al-Shabaab.

"Kuna uwezekano kwamba wao ni sehemu ya bunge na wanafanya kazi humo, wanaweza kuwa wanafanya kazi katika eneo la rais, pia wanaweza kuwa sehemu ya idara ya intelijensia wao wenyewe," alisema.

"Kila kitu kinawezekana kwa sababu wafanyakazi wa serikali hawakuwa wamechunguzwa," alisema.

Alisema vikosi vya usalama na intelijensia vinapaswa kukusanya taarifa "kwa kila mfanyakazi wa serikali", akiongeza kwamba ni muhimu kusaidia washiriki wa umma katika vipengele vyote vya usalama, ikiwa ni pamoja na intelijensia kukusanya na kuwezesha operesheni za usalama.

'Mashambulio yanatukatisha tamaa'
Ahmed Jama Ahmed, mkuu wa mafunzo ya wafanyakazi katika Mashirika ya ndege ya Somalia wakati wa utawala wa Mohamed Siad Barre, alisema ilikuwa ni lawama kwamba mfanyakazi anafanya kazi ndani ya maeneo ya Jumba la kifahari Somalia alihusishwa katika shambulio.

"Sio kawaida kuwa na mashambulio mawili ya al-Shabaab katika nyumba ya rais [wakati] serikali imechukua jukumu la usalama wa taifa na kuwahakikishia watu itatekeleza programu yake mpya ya [usalama], inayoitwa 'Fungua Mfungo Wako kwa Amani,'" aliiambia Sabahi.

"[Mashambulio] yametukatisha tamaa na kutufanya tuamini kwamba utulivu hauwezi kutarajiwa kesho au kesho kutwa," aliongeza.

"Tunahitaji serikali na tunahitaji amani. Hatutaki ugaidi," alisema. "Hata hivyo, swali ni kwamba: Kwa jinsi gani tutaiamini serikali hii kutupatia mahitaji yetu?"

Post a Comment

Previous Post Next Post