WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN
POMBE MAGUFULI AMEFUNGUA RASMI KIVUKO CHA MV MARA CHENYE UWEZO WA
KUBEBA TANI 25 YANI MAGARI MANNE( 4) NA ABIRIA 50 KITAKACHOTOA HUDUMA
KATI YA IRAMBA WILAYA YA BUNDA NA MAJITA WILAYA YA BUTIAMA
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE
MAGUFULI AKITOA MAELEKEZO KWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA UJENZI MHANDISI
MUSSA IYOMBE KUSHOTO HUKU MWENYEKITI WA BODI YA TEMESA HERBERT MRANGO
PAMOJA NA MTENDAJI MKUU WA TEMESA MAMA MARCELINA MAGESSA WAKISIKILIZA
KWA MAKINI.
PICHA YA KIVUKO KIPYA CHA MV MARA KAMA KINAVYOONEKANA KATIKA PICHA KABLA YA KUFUNGULIWA
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE
MAGUFULI AKIPOKEA ZAWADI ZA KIMILA KUTOKA KWA WENYEJI WA BUNDA ZA
KUMTAMBUA KUWA MKAZI WA MJI HUO KWA KIMILA.
WAZIRI WA UJENZI MHE. DKT. JOHN
POMBE MAGUFULI AKIHUTUBIA WAKAZI WA IRAMBA KATIKA JIMBO LA MWIBARA KABLA
YA KUZINDUA KIVUKO CHA MV. MARA CHENYE UWEZO WA KUBEBA TANI 25 YANI
MAGARI MANNE NA ABIRIA 50
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE
MAGUFULI AKIFURAHIA NA WANACHAMA WAPYA WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM
WALIOAMUA KUJIUNGA NA CHAMA HICHO MARA BAADA YA WAZIRI MAGUFULI KUMALIZA
KUHUTUBIA MKUTANO.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE
MAGUFULI KATIKATI AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI WA KIVUKO KIPYA CHA
MV MARA KITAKACHOTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA IRAMBA BUNDA NA MAJITA
MUSOMA VIJIJINI. KUTOKA KUSHOTO NI KAIMU MKUU WA MKOA WA MARA MHANDISI
EVARIST NDIKILO AKIFATIWA NA MBUNGE WA JIMBO LA MWIBARA ALPHAXAD KANGI
LUGORA, WENGINE KUTOKA KULIA NI KATIBU MKUU WA WIZARA YA UJENZI
MHANDISHI MUSSA IYOMBE AKIFATIWA NA MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD
MKONO PAMOJA NA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE
MAGUFULI AKIBONYEZA KITUFE CHA KIVUKO CHA MV MARA KUASHIRIA KUKIZINDUA
RASMI KWA AJILI YA KUANZA KUTOA HUDUMA KATI YA MAENEO YA IRAMBA NA
MAJITA KATIKA WILAYA MBILI ZA BUNDA NA MUSOMA VIJIJINI
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE
MAGUFULI AKIFURAHIA JAMBO NA MWENYEKITI WA BODI YA TEMESA BALOZI HERBERT
MRANGO HUKU MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO ALIYESIMAMA KULIA NA
MBUNGE WA MWIBARA KANGI LUGORA WA KWAANZA KUSHOTO WAKIANGALIA
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIPUNGIA WAKAZI WA MWIBARA MARA BAADA YA KUFUNGUA KIVUKO CHA MV MARA
BAADHI YA WAKAZI WA IRAMBA KATIKA
JIMBO LA MWIBARA WAKIWA WAMEPANDA JUU YA MITI ILI KUMSHUHUDIA WAZIRI WA
UJENZI DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKIHUTUBIA KABLA YA UZINDUZI WA KIVUKO
HICHO
PICHA YA BOTI AMBAYO ILIKUWA IKITUMIKA AWALI KUVUSHA WATU KATI YA MAJITA NA IRAMBA KWA GHARAMA YA SHILINGI 2000/=
……………………………………………………………
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John P.
Magufuli amewataka wakazi wa Iramba na Majita kutunza kivuko kipya cha
MV Mara ili kiweze kuwasaidia katika kuinua uchumi wa maeneo hayo.
Waziri Magufuli alitoa tamko hilo jana kabla ya kuzindua kivuko hicho kipya katika kijiji cha Iramba wilayani Bunda mkoani Mara.
“Ndugu zangu wa Iramba kitunzeni kivuko hiki kwani ni mkombozi
mkubwa katika kuwaletea maendeleo yenu pamoja na maeneo ya jirani”
Alisema Waziri Magufuli
Pia Waziri Magufuli aliwaasa wavuvi kutotega nyavu kwenye njia
za kivuko ili kiweze kudumu kwa muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo
watasababisha injini za kivuko hicho kuharibika mapema.
Aidha Waziri Magufuli aliwapongeza Mbunge wa Mwibara Kangi
Lugora pamoja na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono kwa juhudi zao
zilizochochea kupatikana kwa kivuko hicho.
Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa kivuko hicho chenye uwezo wa
kubeba tani 25, yaani magari manne 4 na abiria 50, kitaokoa maisha ya
wananchi wengi ambao walikuwa wanapata adha kubwa ya usafiri kutokana na
kukosa usafiri wa uhakika ambao ulikuwa unahatarisha maisha yao.
“Nimeambiwa hapa nauli ilikuwa Shilingi 2000/= kuvuka upande wa
pili kwa kutumia boti za watu binafsi lakini kwa kivuko hiki natangaza
rasmi kuwa nauli kwa kivuko chetu kipya ni shilingi 500/= tu, na
wanafunzi waliovaa sare watapanda bure, watoto sh.100” Alisema Waziri
Magufuli
Dkt.Magufuli aliongeza kuwa nauli za magari na mizigo zitapangwa
na Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ambao ndio wasimamizi wa kivuko
hicho.
Aidha, Waziri Magufuli aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu bila kuangalia itikadi zozote za kisiasa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa kijiji cha
Iramba, walisema kuwa walikuwa wanapata taabu sana ya usafiri kwani
ilikuwa inawalazimu kuvuka kwa mitumbwi ambayo ilikuwa inahatarisha
maisha ya wakazi wa maeneo hayo.
Taarifa hii imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Wizara ya Ujenzi
Post a Comment