Donald Musoti.
BEKI wa kati wa Simba, Mkenya Donald Musoti amesema yupo tayari kuvunja mkataba na Simba kutokana na kupata ulaji wa maana nchini Dubai katika Falme za Kiarabu.
Musoti, beki wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya, juzi aliamua kuvunja
ukimya na kufunguka sababu zilizomfanya kuchelewa kuripoti kambini kwa
siku tano, ambapo alisema alikuwa Dubai katika timu hiyo ambayo
hajaikariri jina.
Mkenya huyo ameliambia gazeti hili kuwa meneja wake Michael Msetya,
anashughulikia suala lake la kuvunja mkataba na Simba ambapo umebakisha
mwaka mmoja na nusu.
“Nilikuwa Dubai kuna timu moja nilienda kufanya mazoezi, lakini jina
lake gumu kidogo mpaka niangalie kwenye ‘document’ zangu. Wamesema
Desemba (mwaka huu) ndiyo natakiwa kwenda, tumeshamalizana kila kitu
kasoro mkataba tu.
“Kweli siwezi kuiacha ofa yao, nataka kuondoka Simba,” alisema nyota huyo.
“Kweli siwezi kuiacha ofa yao, nataka kuondoka Simba,” alisema nyota huyo.
Post a Comment