Msanii wa Young Money Nicki Minaj ambaye mwaka 2012 alizindua
manukato ya Pink Friday yaliyopata tuzo amezindua manukato mapya
aliyoyaita Minajesty: Exotic Edition.
Alhamisi iliyopita Nicki Minaj alionekana kwenye kituo cha HSN
akitambulisha mauzo ya kwanza ya perfume hio na siku hio aliweza kuuza
perfume zote alizokuja nazo ambazo zilikuwa chupa 9,000 na mpaka sasa
ameuza chupa 25, 000 na bei ya chupa moja ni dola za Kimarekani 59.50.
Post a Comment