Wabongo wamtaka Rose Muhando amlete Rebecca Malope

MWIMBAJI mahiri nchini, Rose Muhando amesema mashabiki wengi nchini wameomba malkia wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope, awepo kwenye uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu Agosti 3, mwaka huu.

Uzinduzi huo utafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na tayari wasanii mbalimbali nchini wameshaalikwa kushiriki.

“Nimekuwa nikipokea simu nyingi za mashabiki wangu wakitaka nimualike Rebecca, najua kuna gharama zake kubwa, hivyo kwa kushirikiana na wasaidizi wangu tunalifanyia kazi.“Napenda mashabiki wangu wafurahi, lakini pia itategemea ratiba yake naye inasemaje, hivyo kazi kubwa itafanyika,” alisema Rose.

Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo mpya ya Muhando ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook. Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.

Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

Post a Comment

Previous Post Next Post