Polisi
nchini Sudan wanasema kuwa afisaa mmoja wa ubalozi wa Uhispania
amepatikana akiwa amefariki baada ya kudungwa kisu nyumbani kwake mjini
Khartoum.
Afisaa huyo mwenye umri wa miaka 60, alikuwa mkuu wa
kitengo cha kutoa viza katika ubalozi wa uhispania na alikuwa ameishi
nchini Sudan kwa miaka mitatu.Alikuwa anaishi katika mtaa wa Garden City mjini Khartoum na mwili wake ulipatikana mapema Jumatatu.
Polisi nchini Sudan pamoja na maafisa wa wizara ya mambo ya nje wamesema kuwa uchunguzi unafanywa.
Duru za kidiplomasia zinasema kuwa kifo cha afisaa huyo ni kweli kimetokea ila haijulikani nia ya mauaji yake.
Afisaa mmoja nchini Urusi na mkewe walijeruhiwa katika tukio lengine kama hilo lililotokea katika ubalozi wa Urusi mwezi Januari.
Hata hivyo, ni nadra kwa afisaa wa ubalozi kushambuliwa nchini Sudan.
Post a Comment