.jpg)
Na Mwandishi Wetu, Tanga
TIMU
ya Coastal Union ya Tanga leo inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki
na Polisi Morogoro katika uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni siku maalumu
ya timu hiyo "Coastal Union Day
Siku
hiyo pia itakuwa maalumu kwa ajili ya utambulisho kwa wachezaji
waliosajiliwa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara unaotazamiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 20 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Coastal Union, Kassim El Siagi kuwa maandalizi ya kuelekea utambulisho huo yamekamilikwa kwa asilimia kubwa
El
Siagi amesema katika kuelekea siku hiyo maalumu kwa timu hiyo
wataangalia uwezekano wa kucheza na timu itakayotajwa baadae baada ya
mazungumzo kumalizika.
Amesema
siku ya kesho itakuwa ni maalumu sana kwa timu yetu tunatarajia
tutaweza kufanya jambo hilo kwa wanachama,wapenzi na mashabiki wetu ili
waweze kufahamu kikosi chao kabla ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu
Tanzania bara
Akizungumzia
maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligi kuu,El Siagi amesema kuwa
maandalizi kwa timu hiyo yanaendelea vizuri kwa wachezaji kufanya
mazoezi asubuhi na jioni.
Post a Comment