
Rais wa
Marekani Barrack Obama hii leo anatazamiwa kutangaza mpango wake wa
kuwatuma wanajeshi 3,000 nchini Liberia kama njia moja ya kusaidia
katika vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola.
Wanajeshi hao
watasimamia ujenzi wa vituo vipya vya kimatibabu na pia watahusika
katika utoaji wa mafunzo ya kimatibabu kwa wahudumu.Kumekuwa na malalamishi kwamba jamii ya kimataifa imelegea katika harakati za kukabiliana na mkurupuko wa Ebole katika mataifa ya Afrika magharibi.
Zaidi ya nusu ya idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huu ni raia wa Liberia.
Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha kuwa huenda watu zaidi wakazidi kufariki.
Umoja wa Mataifa (UN) unapangiwa kuzungumzia jinsi ya kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika mkutano unaopangiwa kufanyika huko Geneva.
Kulingana na viongozi nchini Marekani, mpango wao wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola unalenga-:
Ujenzi wa vituo vya matibabu 17, kila chumba kikiwa na vitanda kumi.
Usambazaji wa vifaa vya huduma ya afya kwa kila nyumbaKampeni ya kuwahamasisha wananchi kuhusu jinsi ya kuwashughulikia wagonjwa wa Ebola.
Ujenzi wa kituo cha kijeshi cha pamoja mjini Monrovia kitakachotumiwa katika shughuli ya kupokea msaada kutoka kwa jamii ya kimataifa.
Wadadisi wa masuala ya kimatibabu wamepongeza mpango huu wa Marekani huku wengine wakitilia shaka nia ya Marekani nchini Liberia.


Post a Comment