Mkurugenzi
wa shirika la upelelezi la marekani FBI, amesema ofisi imemtambua mmoja
wa wanamgambo wa Islamic State aliyekua ameuficha uso wake aliyehusika
na mauaji ya Waandishi wa habari wa Marekani na mfanyakazi wa shirika la
misaada, raia wa Uingereza.
Shirika hilo halijataja jina na uraia wa mtu huyo, lakini serikali ya London imesema anaonekana kuwa muingereza.
James Comey amesema muuaji ametambulika kwa msaada wa washirika wao wa kimataifa.
Mauaji
ya kikatili yaliyofanyika dhidi ya James Foley, Steven Sotloff na David
Haines yalitolewa kwenye video na kupelekwa kwenye mitandao na
wanamgambo hao wa Islamic State na kuchochea mapambano dhidi ya
wapiganaji wa Jihad.

Post a Comment