Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati)
ameyashambulia vikali makundi ya kigaidi na kitakfiri katika eneo la
Mashariki ya Kati akisema kuwa makundi hayo yanaonyesha picha mbaya kwa
dini tukufu ya Kiislamu.
Sheikh Abdullah bin Zayed Aal Nahyan amesema hayo wakati akihutubia
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani na kuongeza kuwa,
vitendo vya makundi hayo ya kigaidi kama vile kuua watu kiholela, kuua
watu kwa umati, kuteka nyara watu, kuwanyanyasa na kuwakandamiza vibaya
wanawake na watoto wadogo wasio na hatia ni jinai, na kwamba Imarati
inalaani vikali jinai hizo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu vile vile amesema,
uhalifu wa kutisha unaofanywa na makundi hayo unakinzana kikamilifu na
mafundisho ya Uislamu na kwamba makundi hayo yanafanya kosa kubwa
yanapobeba bendera ya dini ili kuhalilalisha jinai zao.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Imarati pia amesema, nchi yake inalaani
mbinu za kudhulma zinazotumiwa na makundi hayo yaliyojipachika jina la
Uislamu kwani jinai na uhalifu wa makundi hayo unapingana kikamilifu na
misimamo ya wastani na kuishi na watu wengine kwa usalama na amani.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
Post a Comment