
Mashirika ya
kisheria nchini Afrika Kusini, yameelezea wasiwasi kuhusu vitisho dhidi
ya jaji aliyetoa uamuzi katika kesi inayomkabili mwanariadha mlemavu wa
Afrika Kusini Oscar Pistorius.
Jaji Thokozile Masipa alimpata Pistorius na hatia ya kuua bila kukusudia wala sio mauaji ya kusudi.
Jaji huyo amekuwa akikosolewa tangu kutoa uamuzi wake kuwa Pistorius alimuua mpenzi wake kwa bahati mbaya.
Baadhi ya matamshi yaliyotolewa ni ya chuki , kumlimbikizia lawama na hata kwenda kinyume na mahakama.
Bi Masipa amewekewa ulinzi tangu kutoa uamuzi wake, kwa mujibu wa jarida la City Press.
Maafisa wa polisi wamekuwa wakishika doria nje ya nyumba yake na pia wamekuwa wakimsindikiza kila anapokwenda.
Pistorius alikana kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kukusudia.
Taarifa
ya wanasheria hao ilisema kuwa uamuzi wa jaji Masipa ilikuwa sawa
kuambatana na sheria na pia kulingana na ushahidi uliotolewa Masipa.Wataalamu
wa maswala ya kisheria wamekosoa uamuzi wa jaji Masipa ambaye alichukua
wadhifa wake mwaka 1998 na kuwa mwanamke wa pili mweusi kuwahi
kushikilia wadhifa huo.
Viongozi wa
mashitaka walilaani uamuzi wa jaji Masipa wakisema kuwa Pistorius
alipaswa kupataikana na hatia ya kumuua mpenzi wake kwa kukusudia.
CREDIT: BBC/SWAHILI
Post a Comment