Kaburi la mmoja kati ya watu waliopoteza maisha katika ajali
mbaya iliyohusisha mabasi ya Mwanza Coach na J4 katika eneo la
Sabasaba, Musoma, Mara limekutwa likiwa limefukuliwa na watu
wasiojulikana leo asubuhi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichofika katika eneo la makaburi ya
Musoma Basi, ndugu wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Juma Sai walienda
asubuhi kuangalia kaburi ikiwa ni siku ya tatu tangu wafanye mazishi,
ndipo walipokuta kaburi limefukuliwa na mbao zilizotumika kuhifadhi
mwili kwa imani ya dini ya kiislamu zikiwa zimewekwa pembeni.
“Mwili wa marehemu bado uko ndani, watu wengi wako hapa na polisi
wameimarisha hali ya usalama. Madaktari wameshafika hapa na wanafanya
uchunguzi kuona kama kuna kiungo chochote kilichotolewa kwenye mwili wa
marehemu. Inasikitisha sana.” Kimeeleza chanzo chetu cha kuaminika.


Ijumaa iliyopita, kulitokea ajali mbaya iliyohusisha magari matatu,
mabasi ya kampuni ya Mwanza Coasch na J4 pamoja na gari dogo aina ya
Landcruiser. Watu zaidi ya 40 walifariki na wengine 79 kujeruhiwa.
Post a Comment