Kampuni
ya Samsung inazindua rasmi duka kubwa na kituo chake cha huduma kwa
wateja lililopo barabara ya Sokoine mjini Arusha siku ya leo. Uzinduzi
huo utawawezesha wateja wake wote mkoani Arusha kupata huduma stahiki na
bidhaa halisi za Samsung. Kituo hiki ni cha kwanza kuzinduliwa mkoani
Arusha na kampuni hii yenye idadi kubwa ya watumiaji na vifaa bora vya
kielektroniki ulimwenguni.
“Mtazamo
wa maisha ya wateja hubadilika kwa kasi kubwa na kuwafanya kuongeza
mahitaji ya bidhaa na huduma bora. Kama kampuni kubwa inayoongoza kuwa
na vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni, Samsung imefanya juhudi
kubwa kuhakikisha inatimiza mahitaji ya wateja wake wote Afrika. Mkoa wa
Arusha hutegemea sana biashara kwani una wakaazi toka jamii
mchanganyiko. Hivyo katika Afrika Mashariki, Arusha ni kitovu cha wageni
toka nchi mbalimbali ulimwenguni. Kampuni ya Samsung ina imani kubwa
kwamba kituo cha huduma kwa wateja kitatoa ushirikiano mzuri na
kuboresha uhusiano kwa wateja wake mkoani Arusha. Kwasababu Arusha ni
kituo kikuu cha safari nchini Tanzania”,haya yamesemwa na Mkurugenzi mkuuwa kampuni hii nchini Tanzania, Bw. Seo
Mbali
na kuuza simu za mkononi na bidhaa za kielektroniki, duka hili jipya la
Samsung litatoa huduma za ziada kwa wateja wake. Hii ni pamoja na
kuwapa wateja wake watakaojisajili na uduma ya e-warranty (dhamana) usaidizi wa kiufundi bila malipo kwa kipindi cha miaka miwili.

Mpango
huu utawanufaisha wateja wa Samsung watakaosajili bidhaa zao kupitia
Simu. Huu ni mchakato utakaofanyika kwa kutuma namba ya IMEI kwenda
15685. Baada ya kufanya hivyo wateja watanufaika na msaada wa kifundi
kwa kipindi cha miaka miwili sambamba na kujipatia nafasi ya kushinda
bidhaa mbalimbali za Samsung.
Katika
kusherehekea uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja ambacho
kinawasogezea wateja wake huduma karibu, kampuni hii kubwa duniani
inawaletea habari njema wakaazi wa Arusha kwa kutoa punguzo kubwa la bei
za bidhaa zake. Kwenye kipindi hiki cha ufunguzi bidhaa zitakazokuwa na
punguzo la bei ni pamoja na; Luninga, feni, majokofu na vifaa vya
nyumbani. Bila kuwasahau wateja wake wa simu, vifurushi vya intaneti na
zawadi za T-shirts zitatolewa kwaajili ya wanunuzi wa simu aina ya
Galaxy Trendlite.
Kwa
sasa nchini Tanzania kampuni ya Samsung ina maduka na vituo vya huduma
kwa wateja katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam na ina mipango
kabambe kuongeza huduma zake mikoa mingine.
Duka
hili na kituo chake cha huduma kwa wateja vitatoa huduma siku za wiki
yaani Jumatatu-Ijumaa kuanzia saa 9.30 asubuhi hadi 5.00 jioni kwa
Jumamosi ni kuanzia saa 9.30asubuhi hadi 1.00 mchana, litafungwa siku za
Jumapili na Siku kuu.


Post a Comment