Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mama
Veronica Simba wa Majengo Mombo wilayani Korogwe wakati alipomtembelea
jimbo la Korogwe vijijini linaloongozwa na Mh. Steven Ngonyani Maarufu
kama Prof. Maji Marefu, katika mradi wake wa kufundisha wanafunzi wa
ushonaji wa nguo akiwa katika ziara yake mkoani Tanga akikagua
utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kuhimiza
wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuhimiza huai wa
chama, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC
Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-MOMBO-KOROGWE)
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo wakati
alipomtembemea mama Veronica Simba katika eneo la majengo mjini Mombo
leo huku wanafunzi wa mama Veronica Simba wakifurahia tukio hilo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo wakati
alipomtembemea mama Veronica Simba katika eneo la majengo mjini Mombo huku mbunge wa jimbo la Korogwe vijijini Mh. Steven Ngonyani akifurahia.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akishiriki ujenzi katika
wa maabara katika shule ya sekondari ya Chekereni mjini wilayani
Korogwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana
na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu kulia na Mrisho
Gambo Mkuu wa wilaya ya Korogwe wakati alipowasili katika shule ya
sekondari ya Cherereni Mombo.
Waandishi
wa habari waliokatika msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Said Mwishehe wa
Jambo Leokulia na David John wa Majira wakizungumza na wanafunzi katika
shule ya sekondari Machewa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza
Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani alipokuwa
akitoa maelezo kuhusu sekondari ya Mashewa wilayani Korogwe, Katikati ni
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu na kushoto ni Mkuu
wa wilaya ya Korogwe Ndugu Mrosho Gambo.
Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani akimimina zege wakati akishiriki katika ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari ya Mashewa huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuhudia tukio hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya w atendaji wa serikali wakati alipowasili katika shule ya sekondari ya Chekereni kukagua mradi wa ujenzi wa maabara ya shule hiyo.
Mmoja
wa wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mjini Mombo leo Bw.Mageda Hamza akiuliza
swali katika mkutano huo.
Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Ndugu Henry Shekifu katikati ni Mnec wa wilaya ya Korogwe vijijini Ndugu Edmund Mndolwa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa
mgolole kama ishara ya heshima ya wasambaa kumkaribisha mgeni shujaa
kwao wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Tanga.
Umati wa watu waliohudhuria katika mkutano huo.
Wananchi waliohudhuria katika kutano huo wakinyoosha mikono yao juu kama salamu kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Mmoja wa masjhabiki wa CCM akionyesha alama ya vidole viwili juu kama ishara ya kukubali jambo katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi wakipungia wananchi
mikono wakati alipowasili katika eneo la mkutano wa hadhara mjini Mombo
leo
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa akizungumza na wana Mombo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mombo leo.
Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mh. Steven Ngonyani akizungumza na wapiga kura wake mjini Mombo Korogwe leo.
Wananchi wakinyanyua mikono yao juu wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya wasichana wa kimasai wakiwa katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi vya ngoma baada ya kuwasili katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mombo leo.

Post a Comment