KINANA ATOA MAONI YAKE BAADA YA WANANCHI WA SCOTLAND KUPIGA KURA YA KUUNGA MUUNGANO

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kata ya Kilangalanga katika viwanja vya shule ya msingi Mtongani,Mlandizi jimbo la Kibaha Vijijini tarehe 20 Septemba 2014.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani alitoa maoni yake juu ya kura iliyopigwa na wananchi wa Scotland kuunga mkono Muungano dhidi ya wale waliotaka kujitenga.

Kinana alisema amekuwa akipigiwa simu siku nzima na waandishi wa habari kutaka kusikia maoni yake juu ya kura iliyopigwa Scotland.

Wananchi wa Scotland wamepiga kura na kuunga mkono muungano wa miaka 307 baina ya nchi hiyo na Uingereza katika kura ya maoni ya kihistoria iliyokuwa ikisubiriwa kuamua iwapo Scotland itajitenga.

“Watu wa Scotland wamezungumza. Tumechagua umoja dhidi ya mgawanyiko na mabadiliko chanya kuliko mgawanyiko usio na maana”.
 

Post a Comment

Previous Post Next Post