|
Baadhi ya Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa
Makampuni mbalimbali ya nchini Marekani waliokuja nchini kwa lengo la
kutizama fursa za uwekezaji . |
|
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini
Washington DC,Suleiman Saleh (katikati) akibadilishana mawazo na
mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua Umeme ya TANASI ,William
Crawford.Ziara hiyo inayo ratibiwa na Ubalozi wa Tanzania,Washington
DC ni ya siku ambapo wageni hao wataembelea sehemu mbalimbali kujionea
fursa za uwekezaji. |
|
Afisa Ubalozi wa Tanzaini ,washington DC
,Suleiman Saleh akizungumza juu ya ujio wa wageni hao 11 kutoka
Marekani ambao wako nchini kwa ajili ya kutizama fursa ya
uwekezaji.Hii ni mara ya tatu sasa Viongozi wa Makampuni mbalimbali
ya Marekani wanafika nchini ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa
Rais Kikwete kutekeleza Dipromasia ya Uchumi. |
|
Rais wa Kampuni ya Ahmed's Moving
Express,Inc ,Ahmed Issa,ambaye pia ni Balozi wa heshima
akizungumza na waandishi wa habari katika hotel ya Mount Meru, jijini
Arusha kuhusu ujio wa Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa makampuni
mbalimbali ya Marekani walioko Tanzania .Issa tayari ambaye ni ziara
yake ya tatu sasa kuja Tanzania tayari ameanza uwekezaji katika sekta
ya Utalii ikiwemo kufungua ofisi ya Utalii Carfonia Marekani
iliyozindiliwa hivi karibuni na Rais JAkaya Kikiwete. |
|
Mtaalamu wa Ujenzi wa nyumba za makazi
,Nishati Erick Nyaren akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio
wao Tanzania .Nyaren yuko nchini kuangalia fursa katika uwekezaji
katika sekta ya Ujenzi. na Miundo mbinu. |
|
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua
Umeme ya TANASI William Crawford akiwa na mjukuu wake Colin Machamsoc
akizungumza na wanahabari kuhusu ziara yao ya siku sita nchini
Tanzania ikiwemo kutembelea vivutio vya utalii vya ,Manyara,Serengeti
na Ngorongoro.Crowford yuko nchini kutizama fursa ya uwekezaji
inayopatikana katika sekta ya Kilimo.
|
|
Mhandisi wa vifaa vya matibabu,Bob Reynolds
akizungumza na waandishi wa habari namna anavyofikiria kuwekeza katika
sekta ya Afya hasa kwa kutizama upatikanaji wa vifaa tiba kama X
Ray,Ultrasound na CT Scan. |
|
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kufua
Umeme ya TANASI William Crawford akiwa na mjukuu wake Colin Machamsoc
wakiwa katika pozi la Picha katika hotel ya Mount
Meru. |
|
Marais,Wenyeviti na Wakurugenzi wa Makampuni
mbalimbali ya Marekani wakiwa katika picha ya pamoja katika hotel ya
Mount Meru jijini Arusha |
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii
kanda ya kaskazini.
Post a Comment